Kukata undugu
Kukata Undugu
KUKATA UNDUGU
MUONEKANO WAKE, SABABU NA NJIA ZA KUTIBU
قطيعة الرحم, المظاهر, الأسباب, سبل
العلاج
تأليف محمد بن ابراهيم الحمد
Mfasiri: Haliymah ‘Abdullaah Husayn
00-Kukata Undugu:
Faharasa
FAHARASA
01. Utangulizi
02. Madh-har ya kukata
undugu
03. Sababu za kukata
undugu
-
Ujinga
-
Udhaifu wa Uchamungu
-
Kibri
-
Kupotea muda mrefu
-
Kulaumu sana
-
Kujikalifisha
-
Kutowajali wanaokuzuru
-
Ubakhili
-
Kuchelewa kugawa mirathi
-
Ushirika baina ya wanandugu
-
Kujishughulisha na dunia
- Talaka
baina ya Ndugu
- Kuwa mbali
na uvivu katika ziara
- Kuwa
karibu katika makazi
- Kutokuwa
na subra kwa Ndugu
- Kuwasahau
baadhi ya Ndugu katika mialiko
- Hasadi na
chuki
- Mizaha
mingi
- Umbeya na
uchonganishi
- Tabia
mbaya ya baadhi ya wake
04. Tiba ya ukataji
undugu
- Ni nini
kuunga undugu?
- Kwa kitu
gani unaunga undugu?
05. Fadhila za kuunga
undugu
06. Vitu vinavosaidia
kuunga undugu
01-Kukata Undugu: Utangulizi
Utangulizi
Shukrani zote njema ni
za Allaah rehema na amani zimuendee Mtume wa Allaah na watu wake, Maswahaba na
waliomfuata, ama
baada:
Kukata undugu ni dhambi
kubwa na kosa kubwa inafungua mafungamano inakata vizuizi inaeneza uadui na
chuki inahalalisha kukatana na kuhamana.
Kukata undugu
kunaondosha mazoea na mapenzi kunaidhinisha laana na kuharakisha adhabu,
kunazuia kushuka rehma na kuingia peponi, na kunakufanya uwe mpweke na dhalili,
pia inakuvutia huzuni zaidi, ikikutokea balaa unategemea kwa nani kheri na wema
inakuzidishia zaidi maumivu.
Dhambi hii Amekemea
Allaah katika Kitabu Chake:
“Basi yanayotarajiwa kwenu
mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?
“Hao ndio Mwenyezi Mungu
Aliowalaani, na Akawatia uziwi, na Akawapofoa macho yao.” Muhammad: 22-23
Amesema Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Haingii peponi mkata
undugu.”
02 - Madh-har Ya Kukata Undugu
MADH-HAR YA KUKATA
UNDUGU
Kukata undugu ni katika
mambo yaliyoenea katika jamii ya Waislam, na haswa haswa katika wakati huu
uliotawaliwa na mada (kupenda mali) kumepungua kutembeleana na kuungana watu
wengi wamepoteza haki hii na kupituka, Allaah ndiye mwenye kutegemewa.
Kukata undugu
kunaonekana kwa njia nyingi watu wengine hawawajui ndugu zao wa karibu kwa
kuwaunga kwa mali au vyeo au tabia inapita miezi na huenda miaka hajawatembelea
wala kuwafanyia wema, kuzidisha mapenzi, au kupeana zawadi au kuwazuilia dhara
au maudhi, huenda yeye mwenyewe akawaudhi kwa maneno au matendo au vyote.
Na kuna watu
hawashirikiani na ndugu zao katika furaha wala kuwaliwaza wala kuwapa sadaka
maskini wao bali utamkuta anawatanguliza wengine katika kuwaunga.
Na katika watu
wanawaunga ndugu zao pindi wakiwaunga na anawakata wakimkata huu si uungaji
bali ni kulipa mema kwa mfano wake na hili linatokea kwa ndugu wa karibu na
wengineo kulipa mema sio kwa ndugu peke yao.
Na muunga undugu wa
kweli ni yule aungae nduguze kwa ajili ya Allaah, wakimuunga au wasimuunge.
Amesema Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa
sallam):
(Sio muungaji kwa kutoa
lakini muungaji ni yule ambaye ukikatwa undugu wake anauunga) Al-Bukhaariy
Na katika ukataji undugu
unawakuta baadhi ya watu ambao Allaah Amewapa elimu na kulingania wa mbali na
anaghafilika na kuwalingania watu wake (nduguze) na hili halitakikani; watu wa
karibu ni bora kwa kuwaamrisha mema.
Anasema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala) kumwambia Nabii wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
sallam):
“ Na uwaonye jamaa zako
walio karibu nawe.” Ash-Shua’raa: 214
Na katika madh-har ya
ukataji undugu unakuta baadhi ya familia kubwa anatokea mwenye elimu au mtu
mwema au mlinganiaji unamuona anakubalika zaidi na kuheshimika na watu wengine
wala hapati katika familia yake ila kukanushwa na kupingwa jambo ambalo
linamshushia utukufu wake kumdhoofisha nguvu zake na kupunguza athari yake.
Na katika madh-har
ya kukata undugu kuwagawanya ndugu na kuvunja nguvu zao.
03 - Sababu Za Kukata Undugu
SABABU ZA KUKATA UNDUGU
1. UJINGA
Ujinga unapelekea kukata
undugu.
2. UDHAIFU KATIKA UCHA
MUNGU (TAQWA)
Itakapodhoofika Ucha
Mungu hajali mtu kukata Aliyoamrisha Allaah kuunga wala hatamani ujira wa
uungaji na hajali matokeo ya ukataji.
3. KIBRI
Baadhi ya watu wakipata
cheo cha juu au akapata nafasi nzuri au akawa mfanyibiashara mkubwa anafanya
kibri kwa ndugu wa karibu; anaacha kuwatembelea na kuwapenda anaona yeye ndiye
mwenye haki na yeye ni bora kutembelewa na kuijiwa.
4. KUPOTEA KWA MUDA
MREFU
Kuna baadhi ya watu
wanawapotea ndugu zao muda mrefu anaanza kusema nitawazuru mpaka anazoea kuwa
mbali nao na anawakata.
5. KULAUMU SANA
Baadhi ya watu
anapofanyiwa ziara na mmoja wa ndugu baada ya kupoteana muda mrefu, anamshushia
mvua ya lawama na amepuuza katika haki yake na anafanya taratibu katika kumzuru
hili linapelekea ndugu kuogopa kumzuru kwani atalaumiwa.
6. KUJIKALIFISHA ZAIDI
Mwingine anapozuriwa na
ndugu anajilazimisha kuliko inavyohitajika na anajitia hasara kwa mali nyingi
anajiandaa kumkirimu na anaweza kuwa hali yake ni duni. Hivyo ndugu anapunguza
ziara anaogopa kumtia nduguye katika matatizo.
7. KUTOWAJALI
WANAOKUZURU
Miongoni mwa watu,
anapotembelewa na ndugu hajali wanapozungumza, hawasikilizi katika mazungumzo
yao, wala hafurahii kuja kwao, wala hawashukuru kwa kuja kwao, hawapokei kwa
furaha, anajivuta jambo linalopelekea ndugu kutomtembelea.
8. UCHOYO NA UBAHILI
Baadhi ya watu Allaah Anapowaruzuku
mali au cheo anawakimbia ndugu, sio kwa kibri, ila anaogopa kufungua mlango na
nduguze wataanza kumtembelea na kutaka msaada au linginelo.
Badala awafungulie
mlango awakaribishe na awahudumie kwa analoweza au kuomba samahani kwa
asiloliweza, bali anawaepuka anawahama ili wasimsumbue kwa kutaka misaada mingi
kama anavyodai.
Ni nini faida
ya mali au cheo akiwanyima nduguze?
Amesema Zuhayr bin Abi
Sulma:
ومن يك ذا فضل فيبخل بفضله
علي قومه يستغن عنه ويذ مم
“Mwenye kuwa na uwezo
akafanya ubahili kwa watu wake, akafaidika nao mwenyewe na kulaumiwa.”
Na uzuri ulioje wa
aliyoyasema Al-Baaruudiy:
فلا تحسبن المال ينفع
اذا هو لم تحمد قراه العشائر
“Usihesabie
(usidhani) mali inanufaisha, ikiwa yeye hatosifiwa na wa karibu”
Na katika yaliyosemwa:
ومن ذا الذي ترجو الأباعد نفعه
اذا كان لم يصلح عليه الأقارب
“Ni kitu gani
tunachosubiria wa mbali kutunufaisha, ikiwa ndugu wa karibu hawawezi
kutunufaisha?”
9. KUCHELEWESHA KUGAWA
MIRATHI
Inaweza kuwa baina ya
ndugu Mirathi haijagaiwa ama kwa uvivu wao au baadhi wana makusudi ya
kuchelewesha au mfano wake.
Kila unapochelewa
ugawaji wa Mirathi na muda kupita, kunaenea uadui na bughdha baina ya ndugu
huyu anataka haki yake katika Mirathi atajirike, mwengine anakufa, na wanapata
tabu walio baada yake kukusanya wakala wapate fungu lao, mwengine anamdhania
mwenzie vibaya, yanazidi matatizo na inaenea kuhamana.
10. USHIRIKA BAINA YA
NDUGU
Mara nyingi ndugu
wanashirikiana katika mradi au shirika fulani bila kuafikiana katika misingi
madhubuti na bila ya kusimamia Ushirika kwa uwazi, bali kwa kuridhishana ya
uongo na kutodhaniana vizuri.
Uzalishaji
utakapoongezeka na kutanuka mzunguko wa kazi, kunazuka hitilafu na ubaya pia
dhana mbaya, na haswa ikiwa wana uchache wa Ucha Mungu na kujitolea au ikiwa
baadhi yao wanang’ang’ania rai zao au upande mmoja ukawa unashughulika zaidi.
Na hapa uhusiano unakuwa
mbaya na kufarakana na inaweza kufikia kushtakiana mahakamani.
Anasema Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala):
“ … Na hakika washirika
wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipokuwa walioamini na wakatenda mema. Na hao
ni wachache…” Swaad: 24.
11. KUSHUGHULIKA NA
DUNIA
12. TALAKA BAINA YA
NDUGU
Inaweza kutokea talaka
baina ya ndugu, yanazidi matatizo baina ya ndugu zao ama kwa sababu
zinazohusiana na talaka au mengineo.
13. UMBALI WA MASAFA NA
KUFANYA UVIVU KATIKA ZIARA
14. KUWA KARIBU KATIKA
MAKAZI BAINA YA NDUGU
Huenda hili
likasababisha kukatana. Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwwaab (Radhiya
Allaahu ‘anhu) amesema:
“Waamrisheni wenye
undugu watembeleane wala wasiwe majirani.”
Ameongezea Ghazaali
kutokana na maneno ya ‘Umar “amesema hivyo kwani ukaribu unaleta msongamano
katika haki na huenda likarithisha chuki na kukatana.”
Amesema Aktham bin
Asw-Swayfi:
“Kuweni mbali katika
majumba kuweni karibu katika mapenzi.”
Kisha kuwa karibu katika
masafa kunaweza kusababisha matatizo, na yanatokea matatizo kwa sababu inaweza
kuwa baina ya watoto mashindano na yanaweza kuhama hadi kwa wazazi, kila mzazi
anajitahidi kumtetea mwanae na kunaanza uadui na mwisho kutengana.
15. UCHACHE WA
KUWASTAHAMILIA NDUGU NA KUWASUBIRIA
Baadhi ya watu hawawezi
kustahamili kitu kidogo kutoka kwa ndugu kosa dogo tu au kulaumiwa na mmoja wa
ndugu anafanya haraka kukatana na kuhamana.
16. KUWASAHAU NDUGU
KATIKA SHUGHULI NA HARUSI
Inaweza kuwa kwa mmoja
wa wanafamilia ana harusi au sherehe fulani, anawaalika ndugu kwa mdomo au kadi
au kwa simu, huenda akamsahau mmoja katika ndugu au huenda aliyesahauliwa ni
dhaifu wa nafsi au ana tabia ya dhana mbaya; anafasiri kusahaulika kwamba
wamempuza na kumdharau anaamua kwa dhana hiyo kuwahama.
17. HASADI
Kuna aliyeruzukiwa elimu
au cheo au mali au kupendwa, na wengine unakuta anawahudumia ndugu zake
anawafungulia moyo wake mwema, kwa hilo huenda baadhi ya ndugu wakawa
wanamhusudu na wanamsababishia uadui na kutia shaka katika uaminifu wake.
18. MIZAHA MINGI
Mizaha mingi ina athari
mbaya,huenda ikatoka neno la kujeruhi kwa mtu, hachungi hisia za wengine,
ikampata mtu anayeathirika haraka, ikazaa chuki bughdha kwa muongeaji.
Na hili linatokea sana
baina ya ndugu kwa kukutana kwao sana.
Amesema Ibn
‘Abdil-Bariy:
“Kundi la Ulamaa
limechukia kuzama katika mizaha, kutokana na mwisho mbaya…”
19. UCHONGANISHI
Katika watu kuna ambaye
katika tabia yake Allaah Atuepushe anaharibu uhusiano ulio baina ya wapendanao,
unamkuta anapupia baina ya wapendanao kuwatenganisha na kuchafua usafi wao, ni
ndugu wangapi wametengana kutokana na mchonganishi, mmbeya.
Anasema Al-‘Aashiy:
“Mwenye kumtii
mchonganishi hatomuachia rafiki hata kama alikuwa ni kipenzi aliye karibu.”
20. TABIA MBAYA KATIKA
BAADHI YA WAKE
Baadhi ya watu wanaweza
kuwa na mtihani na mke mwenye tabia mbaya hawezi kumstahamilia yeyote, hataki
ndugu au yeyote washirikiane naye kwa mumewe, anamzuia akitaka kuwakaribisha,
na wanapomzuru ndugu wa mume haonyeshi furaha, hili linasababisha ndugu
kukatana.
Baadhi ya waume wanampa
uongozi mke akiwaridhia ndugu zake anawaunga na ndugu asiowataka mke anawakata
na huenda akamtii katika kuwakata wazazi.
04 - Tiba Ya Kukata Undugu
TIBA YA KUKATA UNDUGU
Tumeona kukata undugu na
madhara yake na baadhi ya sababu zinazopelekea hilo.
Ikiwa mambo ni hivyo,
hapana budi kwa mwenye akili atahadhari na kukata undugu, na ajiepushe na
sababu zinazopelekea hilo na ajue ukubwa wa undugu apupie sababu za kuunga
achunge adabu zinazopasa kuchunga pamoja na Ndugu.
Ni nini kuunga undugu?
Na kwa vitu gani
inakuwa?
Na ni nini fadhila zake?
Na ni njia zipi na
sababu zinazosaidia hilo?
Na ni adabu zipi
zinapasa kuzichunga pamoja na Ndugu wa karibu?
NI NINI KUUNGA UNDUGU?
Kuunga undugu ni kinyume
cha kuhamana.
Kuunga undugu ni
kuwafanyia wema ndugu wa karibu kwa nasaba au kwa ukwe kuwafanyia huruma upole
na kuchunga hali zao hata wakiwa mbali na wakafanya vibaya au wakakukata.
NI KWA LIPI INAKUWA
KUUNGA UNDUGU?
Kuunga undugu kwa mambo
mengi inakuwa kwa kuwatembelea kuwajulia hali kuwaulizia kuwapa zawadi na
kuwaweka kuendana na daraja zao na kuwapa sadaka mafakiri wao kuwafanyia upole
matajiri wao kuwaheshimu wakubwa kuwaonea huruma wadogo na madhaifu pia
kuwasiliana nao kwa barua simu kuwafanyia ziara kuwakaribisha kuwapokea vizuri
kuwatukuza kuwanyanyua katika mambo yao na kumuunga anayekukata.
Inakuwa pia kushirikiana
nao katika furaha kuwaliwaza katika matatizo kuwaombea dua kuwasafishia vifua
kuwapatanisha waliogombana kuwa na pupa ya kuthibitisha mahusiano kuwatembelea
wagonjwa wao kuwaitikia wito.
Na kubwa katika kuunga
undugu, apupie mtu kuwalingania katika uongofu kuwaamrisha mema kuwakataza
maovu.
Na undugu huu utaendelea
ukiwa mwema wenye kutengamaa.
Ama ikiwa ndugu kafiri
au muovu inakuwa kumuunga kwa kuwapa mawaidha na kuwakumbusha na kujitolea kwa
juhudi katika hilo.
Ukiona wanakupinga au
kukufanyia makusudi au ukijiogopea kupotea nao basi wahame vizuri bila
kuwafanyia maudhi na uzidishe kuwaombea du’aa huenda Allaah Akawaongoza kwa
baraka ya du’aa zako. Na ukipata fursa ya kuwalingania mara kwa mara itumie.
Na inapendezeshwa katika
kuwalingania ndugu na kuwapa nasaha ufanye wema katika kuamiliana nao utumie
upole hikma na mawaidha mazuri wala usiingie nao katika mjadala ila kwa uchache
na kwa wema kwani walinganiaji wengi athari yao katika familia na kabila ni
ndogo. Na hili linatokea kwa walinganiaji hawafanyi upande huu kuwa ni muhimu
kuwalingania ndugu wangetafuta njia wangefaulu na kuwaathiri, mfano
kuwanyenyekea, kuwajali, kuwaunga, kujipendezesha kwao.
Na ni juu ya familia au
kabila wawaheshimu wenye elimu katika familia kuwasikiliza na kutowadharau.
Ikitokea hili katika
familia watakuwa huru katika kupanda kufikia ukamilifu na fadhila.
05 - Fadhila Za Kuunga Undugu
FADHILA ZA KUUNGA UNDUGU
1. Kuunga undugu ni alama ya kumuamini Allaah na siku ya mwisho:
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema, amesema
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Mwenye kumuamini Allaah na siku ya mwisho amkirimu mgeni wake, na
mwenye kumuamini Allaah na siku ya mwisho aunge undugu wake.” Al-Bukhaariy.
2. Ni sababu ya kuzidi umri na kukunjuliwa rizki.
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema,
amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Mwenye kupenda kutanuliwa rizki yake, na azidishiwe baraka katika
umri wake aunge undugu wake.” Al-Bukhaariy
Na kuongezewa umri ni kubarikiwa kupewa nguvu katika mwili akili
kuwa salama na maisha mazuri (chakula bora, hewa safi)
3. Mwenye kuunga undugu anakuwa karibu na Allaah
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Hakika Allaah Ameumba viumbe mpaka Alipomaliza ulisimama undugu,
ikasema; huyu amesimama anajikinga Kwako na anayemkata, Akasema ndio hivi
huridhii Nikimuunga anayekuunga na Ninamkata anayekukata? Akasema sawa.
Akasema hilo lako (umekubaliwa ombi lako).” Al-Bukhaariy.
4. Kuunga undugu ni sababu kubwa ya kuingia peponi
Kutoka kwa Abu Ayuub al-
Answaariy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba mtu alisema;
“Ewe Mtume wa Allaah, nifahamishe tendo litakaloniingiza peponi na
litakaloniepusha na moto.” Akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Umuabudu Allaah wala Usimshirikishe na chochote, usimamishe Swalaah utoe
Zakaah na uunge undugu” Al-Bukhaariy.
5. Kuunga undugu ni katika kumtii Allaah, kwani unafuata
uloamrishwa.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na wale ambao huyaunga Aliyoamrisha Mwenyezi
Mungu yaungwe, na wanaikhofu hisabu mbaya.” Ar-Raa’d: 21
6. Nayo ni katika mazuri ya dini, Uislam ni dini ya kuunganisha
dini ya wema huruma inaamrisha undugu na inakataza kukatana.
Inapelekea makundi ya Waislam wenye kushikamana kuzoeana kuoneana
huruma kinyume na vikundi vingine visivyochunga haki hii wala kutilia umuhimu.
7. Sheria zote za dini za mbinguni zimeafikiana kuhusu kuunga
undugu na kuhadharisha ukataji wake. Na hili linaonesha umuhimu wake.
8. Kuunga undugu kunapelekea kutajwa vizuri na kusifiwa hata watu
wa enzi ya ujahilia (ujinga) walikuwa wanawasifia waunga undugu.
9. Kunapelekea wema na ni dalili ya uzuri wa nafsi na ukweli
katika kuishi na watu. Palisemwa asiyewafaa ndugu zake hawezi kukufaa…
10. Inaeneza upendo baina ya ndugu.
Kwasababu inaenea mapenzi na mazoea mazuri, ndugu wanakuwa kitu
kimoja, hivyo maisha yao yanakuwa safi na furaha inazidi.
11. Kunyanyuliwa muunga undugu.
Mwanadamu akiwaunga Ndugu zake,na akachunga katika kuwatukuza,
watamkirimu, watamheshimu, watakuwa ni wenye kumsaidia.
12. Kuwa na cheo wenye kuungana.
Ndugu wenye kuungana
kupendana wataheshimika kila mtu ataogopa kuwafanyia ubaya kinyume na hivyo
wakikatana kufanyiana vitimbwi watadharaulika watadhalilika baada ya utukufu na
kuwa juu.
06 - Vitu Vinavyosaidia Kuunga Undugu
VITU VINAVYOSAIDIA
KUUNGA UNDUGU
Kuna adabu ziinazopasa
kufuatwa pamoja na ndugu
1. Kufikiria athari
zinazoendana na undugu na mwisho mzuri ni kitu kikubwa inapasa tufuatilie.
2. Kutazama mwisho mbaya
wa ukataji undugu na hilo ni kufikiria yatakayoletwa na ukataji undugu ikiwa ni
pamoja na matatizo, majuto, hasara, n.k. Ukifikiria hayo, itakusaidia uepuke
kukata undugu.
3. Kutaka msaada kwa
Allaah Kwa kumuomba Akuwezeshe katika kuunga undugu.
4. Kubadilisha mabaya ya
ndugu kwa ihsaan. Hili linabakisha mapenzi na linahifadhi yaliyo baina ya ndugu
katika makubaliano. Na linakupunguzia mwanaadamu unayopata katika ubaya wa
ndugu.
Na kwa hilo, alikuja mtu
kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Ewe Mtume wa Allaah,
mimi nina ndugu nawaunga wananikata, nawafanyia wema na wao wananifanyia maovu,
nawa mpole kwao wananifanya mjinga. Akasema “ikiwa uko kama unavyosema
kanakwamba unawalisha majivu ya moto, na hutoacha kuwa unaungwa mkono na
Allaah, ukidumu kwa hilo.”
5. Kukubali udhuru wao
wakikosea au kuomba msamaha.
Na uzuri unaotajwa
katika hilo ni yaliyomfika Nabii Yuusuf na nduguze. Baada ya yote waliyomfanyia
alikubali walipoomba msamaha na akawaombea Allaah Awasamehe wala hakuwagombeza
kwa makosa yao.
6. Kuwasamehe na kusahau
aibu zao hata kama hawajaomba msamaha na hilo linaonesha ukarimu wa
nafsi.
7. Unyenyekevu na tabia
laini
Hilo linapelekea
ndugu kumpenda mtu na kuwa karibu naye.
8. Kufungua macho na
kutoshughulika na mambo mengine au makosa madogo sio kila uonalo unatoa kasoro,
itakufanya ugombane kila mara.
9. Kujitolea kadri ya
uwezo wako ikiwa ni cheo nafsi au mali.
10. Kutotaka wakusifie
au wakulipe mfano wa uliyowafanyia
11. Kutuliza nafsi na
kuridhika na kidogo kutoka kwa ndugu.
12. Kuchunga hali zao na
kujua hisia zao na kuwaweka kuendana na daraja zao. Wako miongoni mwa ndugu
mwenye kuridhia kitu kidogo, inamtosha ukimtembelea mara moja kwa mwaka, au
inamtosha ukiongea naye kwa simu, mwengine inamtosha kwa ukunjufu wa uso na
kuongea naye, mwengine haridhiki mpaka umzuru (umtembelee) mara kwa mara. Hivyo
ishi na mtu jinsi alivyo ili ubakishe upendo.
13. Kuacha kuwabebesha
ndugu wasiyoyaweza na kuwaondolea mazito.
14. Kujiepusha
kulaumu sana.
Mpaka wazoee ndugu
kumijia na kufurahi nae, mkarimu ni yule anayewapa watu haki zake na
ananyamazia haki zake asipotekelezewa. Hata kukiwa na kosa inayohitaji kukemewa
basi iwe kwa upole.
15. Kuvumilia lawama za
ndugu na kuwabeba vizuri.
Mwenye akili na malezi
mazuri anapolaumiwa na mmoja katika ndugu anachukulia vizuri na anaona
anampenda, hivyo anamtaka msamaha kupunguza hasira zake na inaonesha anataka
amtembelee ndio maana analaumu.
16. Kuwa kati na kati
katika mizaha na ndugu kuchunga hali zao na kujiepusha kuwatania wasiopenda
hilo.
17. Kujiepusha na ugomvi
na majadiliano mengi haya yote inarithisha bughdha, ubinafsi na inachafua
mahusiano.
18. Kuharakisha kuwapa
zawadi ikitokea migongano na ndugu. Zawadi zinaleta upendo na kuepusha dhana
mbaya.
19. Aweke akilini
mwanaadamu kwamba ndugu ni pande la nyama kutoka kwake kwa hiyo hana budi kuwa
nao wala hawezi kujivua wakitukuka wao ndio kutukuka kwake wakidhalilika ndio
kudhalilika kwake.
20. Ajue kuwa kuwafanyia
uadui ndugu ni shari na balaa mwenye kufaidika kwa hili ni mwenye hasara na
mwenye kushinda ni mwenye kushindwa.
21. Kuchunga katika
kuwakumbuka ndugu katika sherehe na matukio mbalimbali. inatakiwa mtu aandike
majina na namba za simu za ndugu na azihifadhi ili iwe rahisi kuwakumbuka
anapowahitaji. Na anapomsahau mmoja wao amwendee amwombe msamaha na amridhishe
kadri ya uwezo wake.
22. Kupupia kupatanisha.
Inapasa aliyepata bahati
ya kupendwa katika familia arekebishe panapotokea matatizo kwani mzozo
usiposuluhishwa moto wake utawaenea wote.
23. Kuharakisha kugawa
mirathi.
Ili kila mmoja achukue
fungu lake na kusienee ugomvi na madai na kuwe na mafungamano baina ya ndugu.
24. Kupupia uhusiano
mzuri na maafikiano katika ushirika.
Wakiingia ndugu katika
kushirikiana kila mmoja achunge waelewane katika mambo yao na yawe na kujitolea
na upendo kushauriana na kuhurumiana ukweli na amana na kila mmoja ampendelee
mwenzie analopendelea nafsi yake na kila mtu ajue wajibu wake na wa mwenzie.
Kama inavyopendezwa
wajadiliane matatizo kwa uwazi wapupie kufikia muafaka na ikhlaas katika kazi
na kusamehe vitu vidogo, pia waandike maafikiano yao.
25. Mikutano ya mara kwa
mara.
Iwe kila mwezi au mwaka
kukutana huku kuna kheri nyingi watu wanajuana, wanaungana, wanapeana naswaha
na haswa haswa wasimamizi wakiwa ni wenye elimu.
26. Sanduku la
wanandugu.
Ambalo hukusanywa
michango ya ndugu yenye wasimamizi katika familia ili atakapohitaji mmoja
katika wanafamilia mali kwa ajili ya ndoa au lingine wanafanya haraka kujua
hali yake na kumsaidia; hili linazalisha mapenzi na kuikuza.
27. Kielekezo cha ndugu.
Inapendeza baadhi ya
ndugu waweke kielekezo maalum ndani yake kuna namba za ndugu za simu kisha
ichapishwe na kugawanyiwa ndugu wote, hili linasaidia kuwaunganisha na
inamkumbusha mtu ndugu zake akitaka kuwasalimia au kuwaita katika mjumuiko na
harusi.
28. Tahadhari na kuwatia
uzito ndugu.
29. Mashauriano baina ya
ndugu
Inapendekezwa kwa ndugu
kuwa na kikao cha majadiliano au kuwa na viongozi watakaowaendea wakati wa
tatizo ili wapate wazo moja na linalomridhisha Allaah, inatakiwa viongozi hao
wawe wapole wenye uoni na rai nzuri.
30. Mwisho ichungwe
katika hilo, uwe undugu unawakaribisha kwa Allaah kwa ikhlaas bila
kumshirikisha na kuwe kusaidiana katika wema na Uchamungu. Isikusudiwe ujinga
wa kijahilia.
Mwisho tunamshukuru
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kumtakia rehma na amani Mtume wetu.
Pia nachukua fursa hii
kuwashukuru wote waliosaidia katika kupitia.
Ndugu msomaji
unaruhusiwa kutuma maoni na kurekebisha panapostahili Ukamilifu ni wa Allaah pekee, na kama
tunavyofahamu upana wa Lugha ya Kiarabu na ufinyu wa Lugha ya kiswahili.
No comments