KITABU: ZAWADI YA NDOA

Kitabu Hiki Pia kinaweza kupatikana kwa Pdf Kwa kubonyeza hapa

Zawadi Kwa Wanandoa

Mwandishi: Yusuf 'Aliy Badiwi
Mfasiri: Sa'iyd Baawazir (Abu Arwaa)

NDOA - عقد الزواج


Mkataba wa Ndoa ni dalili tosha inayoonesha kuwepo kwa maelewano na makubaliano baina ya pande mbili, na kuridhiana baina ya mke na mume katika kusimamisha mahusiano ya kisheria baina yao. Huwakilishwa maridhiano haya katika maneno yanayotamkwa na yenye kupita baina ya hawa wenye kuwekeana mkataba huu, na huitwa kuwa ni Ijab na Qabuul

1. Nguzo Za 'Aqd Na Sharti Zake - أركان العقد وشروطه

'Aqd inakamilika kwa kukamilika kwa masharti yafuatayo:

a) Idhini ya Walii.
b) Kuridhika kwa bibi harusi mtarajiwa.
c) Kutimia kwa tamko la ndoa yaani Ijaab na Qabuul (yaani iijab na qubuul iliyounganishwa kwa tamko la ndoa au yenye kufidisha maana hiyo).
d) Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu.
e) Kubalighi na kuwa na utambuzi baina ya wanandoa, hivyo haifai kuwepo kwa ndoa ikiwa mmoja wapo ni mwendawazimu au mdogo kwa umri na bado hajabaleghe.

'Aqd hii inalazimika kwa pande zote mbili husika, ila katika baadhi ya hali kama vile mwanamke kudanganywa na kughuriwa na mwanamme au mwanamme kuoa mwanamke asiyezaa kisha akagundua kuwa hazai na hakujua hilo kabla, katika hali hii anayo haki ya kuvunja 'Aqd.

Na kwa hali hiyo hiyo ni kujionesha mwanamme kuwa ni mchaji Allaah na mtu mwenye msimamo kisha baada ya muda ukadhihirika ukweli kuwa ni muovu na ni mtu mpotevu hana sifa hizo za mwanzo, hapa vile vile itavunjika 'Aqd yao.
Na kwa mfano huo huo ni kuoa kwa mwanamme msichana akitegemea kuwa ni bikra kisha ikadhihirika kuwa sio bikra, au akaona aibu nyingine iliyokuwa ni dhahiri na ya wazi kabisa au maradhi yenye kuchukiza.
Imepokewa kutoka kwa Ka’ab bin Zaid kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alioa mwanamke wa kabila la Banii Ghafaar, alipokwenda kwake na baada ya kuweka nguo zake na kukaa katika kitanda na kuona baina ya kitovu na mbavu weupe ambao ulimuondoa na kukaa mbali nae na kuondoka kitandani, kisha akamwambia: “Chukua nguo zako.” na hakuchukua alichompa  (katika mahari.)” (Ahmad)

Amesema 'Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allahu 'anhu)  kwa yule bwana aliyeoa mwanamke nae (mwanamme) hazai, ‘Mwambie kuwa wewe huzai na mpe uhuru wa kuchagua.’
                                                                                                                                                                   

2. Mahari - المهر

Ulipaji wa Mahari huwa unategemea jamii waliyopo waoaji na huwa haina kiwango maalum. Na huitwa hayo mahari صداقا kwa maana ya kuwa ni dalili ya ukweli wa mtu kutaka kuoa, na huitwa wakati mwingine kuwa ni نحلة kwa maana ya kipewacho mtu kisichokuwa na mbadala, na huitwa wakati mwingine kuwa ni حباءkwa maana ya anachopewa mtu katika mali ili kumkirimu sahibu yake, au huitwa kuwa ni علاقة yaani chenye kuunganisha baina ya wanandoa wawili.


Ndoa katika Uislam haiwi ila kwa Mahari, kwa dalili ya neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :
وآ توا النساء صدقاتهن نحلة
“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)

Na Akasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  katika Surat Al-Ahzaab:
يا أيها النبي إنا أحللنا لك أزواجك اللاتي آتيت أجورهن
“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-Ahzaab: 50)

Na Akasema vile vile katika Surat An-Nisaa:
فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة
“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)

Uislam haukupanga malipo maalum ya mahari, cha kuzingatia hapa katika mahari ni maridhiano ya pande mbili husika, lakini kinachopendeza ni kuwa iwe hafifu na kinachowezekana bila ya taklifa kwa yule muoaji.

Imepokewa kutoka kwa Aamir bin Rabia kuwa mwanamke wa kabila la Banii fazara aliolewa kwa Ndara mbili, akasema Mtume (Swalla AAllaahu 'alayhi wa sallam):

أرضيت عن نفسك  ومالك بنعلين؟  فقالت : نعم , فأجازه

“Je, kwa Nafsi yako na kwa mali yako umeridhika kwa ndara mbili? yule mwanamke akajibu: ‘ndio’, akamkubalia.” (At-Tirmidhiy)

Kutoka kwa Sahl bin Saad kuwa Mtume (Swalla AAllaahu 'alayhi wa sallam)  alimjia mwanamke akamwambia:
Ee, Mtume wa Allaah mimi nimeitoa Nafsi yangu kwako, baada ya kusema hivyo ikawa taabu kubwa (kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ), akasimama mtu akasema, ‘Ee, Mtume wa Allah niozeshe mimi kama wewe huna haja nae’, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ,  ‘Je, una chochote cha kutoa sadaka?’ akajibu mtu yule: ‘Sina isipokuwa ni hili shuka langu ninalojifungia,’ akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) , ‘Ukimpa hii shuka yako utakaa bila kuwa na shuka ya kutumia, tafuta kitu kingine,’ akasema mtu yule, ‘Sina kitu kingine.’ Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kumwambia mtu yule, ‘Tafuta walau pete ya chuma’, mtu yule akatafuta na hakupata kitu, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kumwambia mtu yule, ‘Je, umehifadhi chochote katika Qur’an?’ Akasema mtu yule, ‘ndio, sura kadha na kadha, na akataja sura hizo.’ Hapo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema, ‘Nimekuozesha kwa hicho ulichokuwa nacho katika Qur-aan.’”
(Al-Bukhaariy na Muslim)

Imepokewa kutoka kwa Anas, kuwa Aba Twalhah alimposa Umu Sulaym, akasema Umu Sulaym kumwambia Aba Twalhah, Wa-Allaahi! mfano wako harejeshwi, lakini wewe ni kafiri na mimi ni Muislamu, na haiwi halali kwangu kuolewa nawe, ukisilimu hiyo ndio mahari yangu, na sitotaka kingine zaidi ya hilo. Na hiyo ndio ikawa mahari yake (baada ya kusilimu Aba Twalhah).

Hadithi zote hizi za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  zilizotangulia zinakubali mahari hata ikiwa ni ndogo kiasi gani.

3. Kutanguliza Na Kuchelewesha Mahari - المعجّل والمؤجّل

                                                                                                                                                                  


Inafaa na inajuzu kutanguliza na kuchelewesha mahari. Kulipa mwanzo na nyingine kuchelewa kama ilivyo kuwa ni ada na desturi ya mahala na uwezo wa mtu.


Lakini kinachofaa zaidi ni kutanguliza chochote kwa yaliyopokewa na ibn Abbas kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alimkataza Ali kumuingilia bibi Fatma mtoto wake hadi awe ametoa chochote katika mahari. Ali (Radhiya Allaahu 'anhu)  akasema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) , ‘Sina chochote’. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : ‘Liko wapi deraya lako la kihutwamiyya?’ Akampa ikawa ndio mahari yake.” (Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ahmad)

Na akasema bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) : “Ameniamrisha mimi Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) nimuingize mwanamke kwa mumewe kabla hajampa chochote.” (Abu Daawuwd)


                                                                                                                                  

4. Chombo - الجهاز


الجهاز ni kutayarisha anachokihitaji bibi harusi katika vyombo vya nyumbani kama vile fanicha ili aweke nyumbani kwake. Kilichozoeleka ni kuwa Bibi harusi na ndugu za bibi harusi ndio wenye kutayarisha vyombo hivyo na kuvipanga na kuitengeza nyumba, na wengineo huwa wana tabia ya kuvionyesha vyombo hivyo kwa sherehe na hafla za wazi. Leo hii sherehe kama hizi zinaishia katika mitaa wanayoishi watu wa hali ya chini, ‘Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alimtayarishia vyombo bibi Faatwimah ndani yake pana nguo zilizofumwa kwa manyoya ya mbuni, na kiriba cha kuwekea maji na mto wa kulalia uliowekewa mmea wenye harufu nzuri.’ (An-Nasaaiy).

Mwanamme huwa ndie muhusika haswa wa kukamilisha kinachohitajika katika nyumba kama vile vyombo na vitu vingine vya ndani ya nyumba. Kishari'ah hakuna uhusiano wa vitu hivyo na mwanamke, ila alichokipenda kukifanya yeye mwenyewe kwa mapenzi yake.

Share

5. Kumuusia Mke - استحباب وصية الزوجة


Anas amesema: walikuwa Masahaba wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  anapoelekea mke kwa mumewe, wanamuhimiza katika kumuhudumia mumewe na kuangalia na kuchunga haki zake.

6. Wasia Wa Baba Kwa Binti Yake - وصيّة الأب ابنته

'Abdullaah bin Ja'far bin Abi Twaalib amemuusia binti yake kwa kumuambia, ‘Ole wako na wivu, nao ni ufunguo wa Talaka. Na ole wako na malalamiko mengi, nayo hupelekea katika bughudha. Na jitie wanja kwani huko ndiko kujipamba kuzuri zaidi. Na kizuri katika vizuri zaidi ni Maji.’

7. Wasia wa Baba kwa Mkwe Wake - وصيّة العم لصهره

'Aliy bin Abi Tawalib (Radhiya Allaahu 'anhu)  alipo posa kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kumposa mtoto wake Fatma, alisema Mtume juu yake sala na salamu:
"هي لك على أن تحسن صحبته"
“Huyo ni wako maadamu utaufanyia uzuri usuhuba wake.” (Imepokewa na Abu Na'iym)

Na 'Uthmaan bin Anbasa bin Abi Sufyaan akaposa kwa 'Ami yake 'Utbah kutaka kumuoa binti yake, akamkalisha ubavuni mwake na akaanza kupangusa kichwa chake, kisha akamwambia,  ‘Mtu wa karibu zaidi (ndugu) amemposa ninayempenda zaidi, siwezi kumrudisha, na sina sababu ya hilo. Nimekuozesha nawe ni azizi kwangu zaidi kuliko binti yangu, naye moyo wake umegandana nami zaidi kuliko wako, hivyo mkirimu na ulimi wangu utaona tamu kukutaja, wala usimshushie hadhi yake ikapungua hadhi yako kwangu, na nimekuweka karibu pamoja na ukaribu wa udugu tulionao, hivyo basi usiupeleke moyo wangu mbali na moyo wako.’

8. Wasia wa Mume kwa Mkewe - وصية الزّ وج إلى زوجته

Amesema Abu Dardaai kumuusia mkewe: ‘Ukiniona mimi nimekasirika jaribu kuniridhisha, nami nikikuona umekasirika nitakuridhisha, vinginevyo hatutoweza kukaa pamoja.’


Na akasema mmoja wa waume kumwambia mke wake:


Chukua msamaha wangu yatadumu mapenzi yangu (mawadda),


Wala usizungumze katika kilele cha ghadhabu


pindi ninapo ghadhibika.


Wala usinigonge kwa mgongo wako hata mara moja


Kwani wewe hujui ni wapi jua linapozamia


Na wala usizidishe malalamiko na nguvu kuondoka


Na moyo wangu ukakukataa, na mioyo hugeuka


Nami nimeona mapenzi katika moyo na maudhi vile vile


Zikikutana, basi mapenzi hayakai yataondoka.

9. Usia wa Mama kwa Bintiye - وصيّة الأم لا بنت

Amru bin Hujri aliposa kwa Malik kan-da, kumposa Ummu Iyaas binti Auf bin Muhalim Asshaybaniy, na ilipofika siku ya sherehe ya ndoa yake Mama yake Umama bint al-Harith alichepuka nae pembeni na kumuusia,





‘Ee, Binti yangu: hakika usia ukiachwa kwa fadhila ya adabu (yaani isingekuwa na haja ya kuwausia wenye adabu nzuri) ningeliacha kwako, lakini usia mwanangu ni ukumbusho kwa msahaulifu, na msaada kwa mwenye akili. Na lau kwamba mwanamke asingemuhitajia mume basi wazazi kadhalika wasingehitajika. Ni muhimu sana haja zao kuwa pamoja, basi mimi ningekuwa ni mtu nisiyemhitajia baba yako, lakini mwanangu wanawake kwa wanaume wameumbiwa, na wao wameumbwa kwa ajili ya wanaume.


Ee, Binti yangu: Hakika wewe unaacha mazingira uliyoyazoea na unaacha maisha uliyokulia, unakwenda usipopajua na mwenza usiyemzoea, na atakuwa ndie mwangalizi wako, hivyo basi kuwa kwake kijakazi nae atakuwa ni mtumwa wako asiyetamani kukukosa. Hifadhi kwake mambo kumi, atakuwa kwako hazina: 
1) Unyenyekee kwake kwa kukinai.


2) Umsikilize vizuri na kumtii.


3) Na uangalie maeneo ya macho yake na pua yake.


4) Hivyo basi, macho yake yasione au kuangalia yanayochukiza kwako na wala yasinuse ila harufu nzuri kutoka kwako.


5) Angalia wakati wake wa kulala na chakula chake.


 6) Kwani hakika mbabaiko wa njaa unaunguza na kukosa usingizi kunaghadhibisha.


 7) Chunga mali yake na ulinde heshima yake na watoto wake.


 8) Na matumizi ya mali yawe mazuri na katika kuishi nae upange vizuri maisha.


9) Usimuasi kwa jambo na usitoe siri zake.


10) Kwani wewe ukikengeuka na amri yake utapandisha chuki na hasira katika kifua chake, na ukitoa siri zake hutosalimika kwa kumvunjia ahadi yake, kisha ole wako na kufurahi hali yakuwa hana raha, na kukasirika hali ya kuwa amefurahi. 
                                                                                                                                                                  

10. Kutangaza Ndoa - إعلان الزواج

Inapendeza kutangaza ndoa kishari'ah kwa kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :
أعلنوا هذا النّكاح , واجعلوه في المساجد
“Tangazeni ndoa hii, na ifanyeni Msikitini.”
(At-Tirmidhiy na Ahmad)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema tena:
فصل ما بين الحلال والحرام الدّفّ والصّوت
“Mpaka wa baina ya halali na haramu ni dufu na sauti.”
(At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)

Na inawezekana kutangaza ndoa Msikitini kwa sharti ya kuwa mas-alah ya kuimba na dufu yawe nje ya Msikiti ili kuchunga adabu za Msikiti. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alikuwa akichukia sana ndoa kufanywa siri hadi ipigwe dufu na isemwe: “Tumewajia tumewajia, tusalimieni nasi tuwasalimie.”(Ahmad)

Na si vibaya kusheherekea ndoa kwa kuimba kwa lengo la kuzichangamsha nafsi, kwa sharti kuwa nyimbo hizo ziwe zimeepukana na matusi na uchafu wa maana mbaya na pia ni lazima ziwe nzuri zisiwe zenye kuhamasisha matamanio na kuwatoa watu haya.

Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  alisherehekea harusi ya al-Farigha bint Asad na akamsindikiza hadi kwenye nyumba ya mume wake, Nabiit bin Jaabir al-Answariy. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akauliza kumuuliza bibi 'Aaishah:
يا عائشة , ما كان معكم لهو؟ فإنّ الأنصار يعجبهم اللّهو
“Ee 'Aaishah, je, hamkuwa na Lahwu (kucheza na kujipumbaza)?! Kwani Answaar huvutiwa na Lahwu.” (Al-Bukhaariy)

Hali kadhalika imepokewa na bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  amesema: “Hukumfanyia fulani-kwa mayatima waliokuwepo kwake.” nikajibu: tumempeleka kwa mumewe, akasema: “Je, mlikwenda pamoja na kijakazi akapiga dufu na kuimba”, bibi Aisha akasema  aseme nini? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema: “Aseme:

أتيناكم    أتيناكم            فحّيونا  نحيّيكم


ولولا الذّهب الأحمر          ما حلّت بواديكم

ولولا الحنطة السّمرا      ما سمنت عذاريكم


Tumewajia tumewajia,
Tusalimieni tuwasalimie
Na kama si dhahabu nyekundu
Msingeacha vijiji vyenu
Na kama si ngano nyeusi              
Basi wasingenenepa binti zenu

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik amesema: “Alipita Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  mwanzoni mwa kuhamia kwake Madiynah akiwa na harusi pamoja na wanawake, na mmoja wao alikuwa akisema:
Na akazawadiwa Kondoo              akipiga ukelele mkubwa kabisa
Na mumeo yupo Shamba               na unajua ya kesho.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema:  “Usiseme hivyo bali sema:

أتيناكم    أتيناكم            فحّيونا  نحيّيكم
Tumewajia tumewajia,  Tusalimieni tuwasalimie


11. Yachukizayo Kwenye Sherehe ya Harusi - منكرات الأفراح

  • Katika jumla ya mambo yenye kuchukiza katika sherehe ya ndoa ni kuzidi kwa ala za muziki, na nyimbo mbaya chafu za matusi zenye kuchochea hisia za chuki na ngono zenye kuimbwa na watu waliobobea katika maasia. Kisha kibaya zaidi ni ule mchanganyiko wa wanawake na wanaume ambalo ni jambo lisilo la lazima kabisa katika sherehe na haswa zaidi za harusi. Kadhalika kuingia kwa wapiga picha na wapiga ngoma na wachezaji wake kwa Bwana na Bibi harusi na kuwaona wanawake na fitna (mapambo yao) zao na kudhihirika uchi wao mbele yao, hivyo basi kupelekea kudhihiri kwa makosa katika mazingira yaliyotawaliwa na shetani.


  • Na katika jumla ya machukizo ni upigaji wa honi za magari na mazumari mabarabarani, jambo lenye kusababisha kuamsha na kuwastua waliolala, wagonjwa na wanafunzi waliopo madarasani.


  • Na mengine yenye kuingia katika machukizo ni ile ada chafu na mbaya ya kujifakharisha baina ya watu iliyopo katika baadhi za sehemu, kwa mfano mmoja wao kusema: Shabbash kwa Fulani, na anaanza kutaja mali alizotoa katika kuchangia harusi, na anatokezea mwingine anayehamasika na anatoa zaidi ya yule wa mwanzo kwa lengo la kujifakharisha na kujitukuza na kujiona mbele za watu.


  • Na katika yasiyopendeza ni kuingia kwa Bwana harusi ndani kwa Bibi harusi na kukaa nae pembeni, katikati, ya wanawake wasiojisitiri, wenye kujionesha, na haingii peke yake bali ataingia na nduguze wengine.


  • Na mengineyo katika hayo ni ulipuaji wa fataki na baruti eti kudhihirisha furaha yao na kuonekana washiriki wazuri wa harusi ile. Huu ni ujahili na upotefu, je, ni Mabwana harusi wangapi na Mabibi harusi wangapi ambao harusi zao ziligeuka kuwa ni khitma kwa hayo na Mabwana harusi wengine kuingizwa jela na si kuingia kwa mkewe!!.


  • Hali kadhalika mandhari ya sherehe yanapoonyesha ufakhari na kujiona na israfu na kujikalifu kwa taklifa zisizokuwa za msingi na ambazo anagharimika kwazo Bwana harusi kwa taabu ni katika mambo yenye kuchukiza katika sherehe za harusi.


  • Uvaaji wa kupita mipaka kwa wanawake kwenye sherehe za harusi na utengenezaji wa nywele na kujifananiza na wasiokuwa Waislamu, yote haya yanagharimu fedha nyingi sana mbali na uchafu unaoenezwa na fitna za hali hizi.

12. Karamu ya Harusi (Walima) - الوليمة

Walima ni Sunnah iliyokokotezwa kwa neno lake Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam)  kwa A'bdur-Rahmaan bin 'Awf:

أولم ولو بشاة 
“Tufanyie Karamu walau kwa mbuzi mmoja.” (Ahmad)

Na Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam)  amesema vile vile:
                  
إنه لا بدّ للعرس من وليمة
“Hakika katika harusi hakuna budi kufanywa karamu.”(Ahmad)

“Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) aliwafanyia karamu baadhi ya wake zake kwa vibaba (Mudain) viwili vya shairi.” (Al-Bukhaariy na Ahmad)

Ama tofauti ya aina ya chakula kinachotumika katika karamu hutegemea desturi za watu na ada zao na uwezo wao wa kifedha. Ni wajibu wa mwenye kualikwa katika karamu kuitikia mwito huo ili kuingiza furaha kwa wale waliomwalika. Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) amesema:

إذا دعي أحدكم إلى وليمة فليأتها 
“Anapoalikwa mmoja wenu katika karamu na ahudhurie.”
 (Al-Bukhaariy na Muslim)

Na katika hadithi nyingine Mtume juu yake sala na salamu anasema:
من ترك الدّعوة فقد عصى الله ورسوله
“Atakayeacha kuitika mwito basi atakua amemuasi Allah na Mtume wake.”(Al-Bukhaariy na Muslim)

Na Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam)  amesema vilevile:
“Lau ningealikwa kwenda kula kongoro basi ningelikwenda, na lau ningalipewa zawadi ya mkono ningalipokea.” (Al-Bukhaariy)

Inapendeza wale ambao wataalikwa kwenye karamu wawe ni mafakiri na pasiwepo katika karamu hiyo Munkaraat (ubadhirifu na Israfu), Mtume wa Allaah juu yake Swalah na amani anasema:

شرّ الطّعام طعام الوليمة يدعى لها الأغنياء ويترك الفقراء
“Chakula kibaya zaidi ni karamu ambayo wanaalikwa matajiri na kuachwa mafakiri.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Na mwaliko huo unapendeza zaidi uitikiwe na waja wema wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  kwa neno Lake Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) :

لا تصاحب إلاّ مؤمتا ولا يأكل طعامك إلاّ تقيّ  
“Usisuhubiane ila na muumini tu, na asile chakula chako ila Mchaji Allaah.” (Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy)

Matajiri wanahamasihwa washiriki katika kutengeneza chakula cha mafakiri, kwani amesema Anas (Radhiya Allaahu 'anhu)  katika kisa cha Ndoa ya Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam)  kwa bibi Swafiyah, hata ilipofika njiani Bibi Sulaym alitayarisha chakula na akakipeleka usiku, na ilipofika asubuhi yake Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam)  akasema: “Atakayekua na kitu basi aje nacho.” Anas anasema: “Habari zikaenea vitu vikawa vingi! Ikawa kila mmoja anakuja na kitu, wengine walileta samli wengine tende wakatengeneza hays (aina ya chakula kama ugali wa tende uliochanganywa na samli) ikawa wanakula kutokana na chakula kile na wanakunywa katika zile hodhi waliokinga katika maji ya mvua, na hiyo ndio iliyokuwa karamu ya Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) .” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Na du'aa inayosomwa kwa Bwana harusi wakati mtu anapohudhuria karamu ni:
                                                                                                                                                                      بارك الله لك, وبارك عليك, وجمع بينكما في خير
“Allaah Akubariki na Akubarikie mke huyo na Awakusanye pamoja katika kheri.” (Abu Daawuwd)

Mtume juu yake sala na amani amekataza kupeana pongezi za kijahilia. Hasan bin 'Aqiyl bin Abi Twalib alioa kisha watu wakaingia (kumpongeza) wakisema: upate utajiri na watoto, Hasan (Radhiya Allaahu 'anhu)  akasema msiseme hivyo, kwani Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam)  amekataza hilo. (Ibn Maajah, Ad-Daarimy na Ahmad)

Inapendeza kuwaombea dua wanandoa wawili kwa kusema:
على خير والبركة وعلى خير طائر
“Katika kheri na baraka na katika kheri ya kuwa na bahati nzuri na hadhi yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

اللهّم بارك فيهما, وبارك لهما في بنائهما  
“Ee, Allaah! Wabarikie kwa hayo, na uwabarikie wote wawili katika mjengo wao.” (Atw-Twabaraaniy)

SIKU YA MWANZO YA NDOA - ليلة الزّفاف

     Siku hii ndio siku ya mwanzo ya ndoa, ni siku ambayo yenye athari kubwa katika maisha ya Mwanamme Bwana harusi na Mwanamke Bibi harusi kwa matokeo yoyote ya matendo ya siku hii.





Ni vizuri na muhimu sana kwa siku hii ya leo kwa mume kumfanyia upole mkewe na kuzungumza nae na kumzoea na kumuondoa khofu, na vizuri washauriwe wanandoa hawa wapya kuwa na utulivu na wasiwe na pupa yoyote ya jambo, maisha ni marefu na yana wasaa na siku zinakuja hakuna haja ya haraka.





Katika siku hii muhimu sana kwa wanandoa hawa ni vizuri kuchunga miiko ifuatayo:
                                                                                                                       

1. Kumfanyia Upole na Kumlainisha Mkeo - ملاطفة الزوجة

Mume anapoingia kwa mke wake katika siku hii muhimu katika m'Aaishah ya ndoa mara nyingi hisia za khofu na wasiwasi za mwanamke zinakuwa juu, hivyo basi ni juu ya mwanamme kukaa nae kwa upole na kumbembeleza hadi nae ajihisi anaanza kuzoea hali hiyo na kupunguza khofu na wasiwasi aliokuwa nao juu yako. Hekima itumike, ugomvi, matusi au kupiga si mahali pake kabisa, na sio lazima kumuingilia usiku ule ule, unaweza kusubiri hadi asubuhi au hata siku ya pili, mara nyingi mwenye pupa huwa anakosea na matokeo yake yanakuwa ni mabaya (na yenye kudumu katika m'Aaishah mazima ya ndoa yenu).

Imepokewa kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd bin as-Sakan amesema: “Nilimuendea Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  hali ya kuwa amejipamba kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallamnikamuondoa khofu. Baada ya muda kidogo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akaja pembeni yake na kikombe cha maziwa, akayanywa kidogo kisha akampa Bibi 'Aaishah nae akateremsha kichwa chake kwa kuona haya. (Asmaa) nikamnyanyua ('Aaishah), nikamwambia: chukua kutoka kwa mkono wa Mtume wa Allah. ('Aaishah) Akachukua na kuyanywa, kisha (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamwambia, “Wape marafiki zako wa umri wako.” (Ahmad)

Na si neno kwa mke kumkatalia kidogo mumewe kwani katika hilo mtu husisimkwa, na hujitayarisha, na kunapelekea kumjali zaidi na kumtaka. Na kunanasihiwa kwa wanandoa kuwa ni vizuri wakavua nguo zao zote kama vile mshairi anavyosema:

Na tahadhari kuingiliana kunako nguo
Kwani huo ni ujahili usiokuwa na shaka!
Bali kila mlicho nacho – ee, rafiki yangu mkivue
Na uwe ni mchezaji nae ili asifadhaike.

Ni Sunnah mume kusema anapoingia kwa mkewe siku ya mwanzo:
        
  اللهّم إني أسألك من خيرها وخير ما جبلته وأ عوذ بك من شرها وشّر ما جبلتها عليه

“Ee, Allaah nakuomba kheri yake na kheri aliyokuja nayo na uniepushe na shari yake na shari aliyokuja nayo.” (Abu Daawuwd na Ibn Maajah)

Du'aa kama hii hutuliza hisia za mwanamke na Nafsi yake na hukaribisha baraka, na huenda kwa hayo Allaah Akajaalia baraka katika usiku huu.
Share

2. Swalah ya Sunnah kwa Wanandoa - سنّة صلاة الزّواج

Usiku wa mwanzo wa Mume na Mke si kwa ajili tu ya kujifurahisha pekee na raha ya kuingiliana bali ni lazima kutekeleza amri za Dini na katika hayo ni Swalah. Amesema Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) :

إذا تزوّج أحدكم فكانت ليلة البناء فليصلّ ركعتين , وليأمرها أن تصليّ خلفه , فإنّ الله جاعل في البيت خيرا

“Atakapooa mmoja wenu na ikawa ni siku ya mjengo na aswali rakaa mbili na amuamuru mke wake aswali nyuma yake, kwani Allaah Atajaalia katika nyumba hiyo kheri.”
(Imepokewa na al-Bazaar kama ilivyo katika kashfu al-Astaar)

Mtume Amesema juu yake Swalah na amani:

إذا دخلت المرأة على زوجها يقوم الرّجل فتقوم من خلفه فيصلّيان ركعتين ويقول : اللهم بارك لي في أهلي وبارك لأهلي فيّ , اللهم ارزقهم مني , وارزقني منهم , اللهم اجمع بيننا ما جمعت في خير , وفرّق بيننا إذا فرّقت إلى خير

“Atakapoingia mwanamke kwa mumewe, atasimama mwanamme na mwanamke atasimama nyuma yake, na wataswali rakaa mbili na atasema: Ee Allaah! Nibarikie mimi kwa ahli zangu na uwabariki kwangu ahli zangu, ee Allah! Waruzuku wao kwangu na uniruzuku mimi kwao, ee Allaah! Tuunganishe mimi na mke wangu katika muunganisho wa kheri, na Utufarikishe
baina yetu kwa kheri pindi Utakapotufarikisha.”
(Al-Bukhaariy na Muslim)
                                                                                                                                                                   

3. Kinachosemwa Unapomwingilia Mkeo - ما يقال عند الجماع

Mume anaomba anapomuingilia mkewe kwa du'aa aliyofundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :
                           
   بسم الله اللهّم  جنّبنا الشيطان وجنّب الشيطان ما رزقتنا
                                                                                                                           
“BismiLLaah, Ee Allaah, tuepushie sheitani na Umuepushe kwa kile Utakachoturuzuku.” (Al-Bukhaariy na Muslim)
                                                                                                                                  

4. Malipo ya Kuingiliana - ثواب الجماع

Katika kuingiliana hakupatikani kwa raha peke yake bali kunabeba ndani yake malipo mtu anayolipwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  katika kufanya hivyo na mke wake au mume wake, amesema Abu Dharr (Radhiya Allaahu 'anhu) :
Hakika watu katika Maswahaba walimwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  : Ee Mtume wa Allaah wameondoka wenye uwezo (ahlu duthuur) na malipo yote, huswali kama tunavyosali, hufunga kama tunavyofunga, na hutoa sadaka katika bora ya mali zao. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akawaambia, “Je, Allaah Hakuwajaalia katika ya kutoa sadaka? Hakika katika kila tasbiyh (Subhaana-Allaah) ni sadaka. Na katika kila takbiyr (Allaahu Akbar) ni sadaka, na kila tahliyl (La ilaaha illa Allaah) ni sadaka. Na kila tahmiid (AlhamduliLLaah) ni sadaka. Kuamrisha mema ni sadaka na kukataza maovu ni sadaka vile vile na kumuingilia mkeo ni sadaka.” Wakasema Maswahaba na je, katika kupata raha binafsi mmoja wetu analipwa??!. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema: “Je, mnaonaje lau mtu huyo angeingiza (tupu yake) katika haramu, je, ingelikuwa ni shari juu yake (ya madhambi, maradhi, adhabu)?, wakasema: ndio. Akasema  Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : “Hivyo ndivyo atakapoweka (tupu yake) katika halali atalipwa.”  (Muslim)


                                                                                                                              

5. Adabu za Kuingiliana - أدب الجماع

Imepokewa vile vile kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu 'anhu)  kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  amesema:

   إذا جامع أحدكم أهله فليصدقها , فإذا قضى حاجته قبل أن تقضي حاجتها فلا يعجلها حتى تقضي حاجته
“Atakapomuingilia mmoja wenu mkewe na amsadikishe (yaani wote wafikie kilele cha ladha ya kitendo cha ndoa), atakapomaliza haja yake kabla ya mke wake kumaliza ya kwake basi asifanye haraka hadi mke wake nae amalize haja yake.” (Abu Ya'ala)

Tunajifunza katika hadithi hii mafundisho ya kisheria yenye kumtaka mume amsubiri mke wake nae amalize haja yake, amshibishe na afikie kilele kama alivyofika yeye. Mafundisho haya ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) yanatufundisha kujali hisia za mwanamke na kuziheshimu.
                                                                                                                          

6. Kuoga baina ya Matendo ya Ndoa - الإغتسال بين الجماع

'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  amesema: “Atakayemuingilia mke wake kisha akataka kurejea tena katika tendo la ndoa na asafishe tupu yake.” (Atw-Twabaraaniy). 
Kadhalika imesimuliwa toka kwa Abu Rafi kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  siku moja aliwazungukia wake zake, akioga kwa huyu na akioga kwa yule. Nikamwambia (Abu Rafi): Ee, Mtume wa Allah, je, huwezi kujaalia josho moja? Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : “Hivi ni bora, vizuri zaidi na safi zaidi.” (Abu Daawuwd na Ibn Maajah). Katika hadithi nyingine Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  anasema:

إذا أتى أحدكم أهله ثم أراد أن يعود , فليتوضأ بينهما وضوءه للصّلاة
“Atakayemuingilia mkewe kisha akataka kurudi tena (katika tendo la tendo) na atawadhe baina ya matendo mawili wudhuu wa Swalah.”
(Muslim, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)

Katika kuchukua wudhuu, kukosha au kuoga ni katika jumla ya kuchangamsha mwili na kuziibua upya nguvu za kiwiliwili. Na si hivyo tu kunahakikisha usafi katika tendo la ndoa (sexual Hygiene).
                                                                                                                       

7. Adabu za Mtu na Ndugu za Mke Wake - أدب الرّجل مع أقارب زوجته

Katika jumla ya adabu ya mtu na ndugu za mke wake ni kutokutaja maneno au kufanya vitendo vya aina yoyote ile vyenye kuashiria mapenzi ya chumbani kama kubusu na mfano wa hayo, na hii ni katika adabu ya kuishi nao. Imepokewa kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: nilikuwa ni mtu mudhaa-a, nikiona haya kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa nafasi ya mtoto wake kwangu, nikamuomba Miqdaad aniulizie.
                                                                                                                                 

8. Kuharamisha Kuingilia Katika Tupu ya Nyuma - تحريم نكاح الدّبر

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم
“ Wake zenu ni konde zenu, basi ziendeeni konde zenu mpendavyo.”  (Al-Baqarah: 223)

Ilikuwa ni tabia ya Mayahudi wakisema: Mtu atakapomuingilia mke wake mbele lakini kwa upande wa nyuma basi atazaliwa mtoto akiwa ni kengeza; ikashuka Aayah hii: Wake zenu ni mashamba yenu.” (Muslim). Katika riwaya nyingine:

إن شاء مجبّية و إن شاء غير مجبّية غير أنّ ذلك في صمام واحد 

“…na ukipenda ufanye staili ya kama anasujudu na ukipenda sivyo hivyo yote ni sawa sawa...” (Muslim: Hadithi 1435)

Ilikuwa ni tabia ya Ahlul-Kitaab kutomuingilia mwanamke ila kiubavu na katika hali ya mwanamke kujistiri. Na ilikuwa tabia ya baadhi ya Answaar kuiga tabia zao hizo. Na wanaume wa ki-Quraysh walikuwa wamezowea kufanya mapenzi na wake zao vilivyo, wakistarehe nao kwa mbele, nyuma na kwa chali, (lakini bila ya kuwaingilia tupu zao za nyuma). Walipohamia Muhajirina Madiynah alioa mmoja wao mwanamke wa ki-Answaar; akataka kufanya nae mapenzi kwa mitindo waliyozoea (huko Makkah) akachukizwa mwanamke yule na hilo, na akasema: Hakika sisi tulikuwa tukiingiliwa kiubavu, fanya hivyo au niepuke; kisa chao kikaenea, zikamfikia habari Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Allaah Akashusha:
نساؤكم حرث لكم
“Wake zenu ni konde zenu…” (Abu Daawuwd)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema vile vile:
“(Waingilieni wake zenu kwa mtindo wa) Kwa mbele au (kwa mtindo wa) kwa nyuma lakini epukeni dubur (utupu wa nyuma) na (kuwaingilia wakati wako) kwenye hedhi.” (At-Tirmidhiy)
                                                                                                                        

9. Kuoga katika Chombo Kimoja - الإغتسال من إناء واح

Inajuzu kwa wanandoa wawili kuoga pamoja katika sehemu moja, imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  amesema:
Nilikuwa nikioga mimi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  katika chombo kimoja, inapishana mikono yetu ndani yake, na ananianza kwa hilo hadi nasema: niachie … niachie. Akaendelea kusema Bibi 'Aaishah wakiwa hivyo hali ya kuwa ni wenye janaba.” (Muslim)
                                                                                                                                 

10. Kuondosha Bikira - فض غشاء البكارة

Utando wa bikira unatofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine, baadhi yao bikira zao ni khafifu hukatika na kuachia mara moja kwa kuanguka, na baadhi nyingine ni ngumu. Hivyo basi anatahadharishwa mume katika kufahamu na kujua kuwa ule utando wa bikira wenyewe ndio kipimo cha usafi na utukufu wa mwanamke. Katika ada zilizo mbovu kabisa ni ile hali ya baadhi ya wanaume kuondosha bikira kwa kutumia vidole vyao, na haya ni madhara makubwa kwa mwanamke na humsababishia maudhi mengi.







Jambo jingine ambalo ni baya ni zile hila za kisheitani wanazotumia baadhi ya wasichana wasiojitunza na ambao wanawahadaa waume zao siku ya mwanzo ya harusi kwa hila zenye kufahamika na madaktari na makungwi.







Jukumu kubwa linaloonekana kwa waume wengi ni kuondosha utando wa bikira siku ile ile ya mwanzo kwa njia yoyote na husubiri mke wake ajisalimishe kwake kwa hilo. Na wakati mwingine msichana al-huyiyya (bado hajamuona mwanamme) anaweza kukataa na baadhi ya wasichana hufikiri kuwa ndoa ni mchezo na matembezi hivyo basi akimuona mwanamme amevua nguo zake na uume wake umesimama akiwa ni mwenye pupa na jambo lake huanza kuogopa na huenda akaupiga ukelele na hujaribu kujizuia na mume wake na hii inarejea na uduni wa uzoefu wa wote wawili mume na mke na kuwa na fikra mbovu kuhusu ngono.



                                                                                                                                                              

KUMCHEZEA MKE- مداعبة الزّوجة

Hakika katika jambo ambalo ni muhimu kwa mume kulichunga na kulilinda ni kumchezea chezea mke wake na haswa kabla ya kumuingilia, hili lina athari kubwa sana kati ya wanandoa wawili katika mahusiano yao ya kiroho na ya kijinsi.

Katika kufikia kilele cha raha ya kiwiliwili kunahitaji kwa mwanamme awe na diplomasia ili aweze kumpa mke wake hamu na matamanio ya kweli, na ushiriki mzuri ulio kamili na mapenzi yaliyokita.

Mke mwenye hekima anaweza kwa diplomasia aliyokuwa nayo na mapambo yake na usafi wa kiwiliwili chake kumvuta mume wake na kumtamanisha. Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa kiwiliwili vyao kwa urahisi na wepesi zaidi, mahaba siku zote yanatimiza furaha.

Ama kumuingilia mwanamke bila ya kuwepo vitangulizi huwa ni jambo lisilofaa na la kinyama la kutosheleza mahitaji ya mwanamme, kisha haupiti muda mrefu kamaliza haja na kukaa mbali ya mwanamke hali ya kuhema!.

Mwanamke siku zote hupendelea mumewe ashirikiane nae katika hisia zake kwa upole na wema na acheze nae kwa muda unaotosha kupandisha hamu na nyege zake. Na hivi vitangulizi vya jimai husaidia kuwafikisha wanandoa wawili katika utulivu kamili na hivyo kufikia kilele cha raha ya tendo la ndoa.

Kwa hilo na mengineyo Uislamu unahimiza suala hili la kuchezeana na kumchezea mke, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :


كلّ شيئ ليس من ذكر الله , لهو ولعب إلاّ أن يكون أربعة: ملاعبة الرّجل امرأته و تأديب الرّجل فرسه ومشي الرّجل بين الغرضين وتعليم الرّجل السّباح

“Kila kitu katika lahau na mchezo si katika dhikri ya Allah ila iwe ni kimoja katika hivi vinne: 1)  Mwanamme kumchezea mke wake. 2)  Mtu kumfundisha farasi wake. 3) Na mtu kutembea katika kamba mbili za juu au milingoti miwili. 4) Na mtu kujifunza kuogelea.” (At-Tirmidhiy)

Na katika kuchezeana suala muhimu ni upole na ulaini na kumsubiri mkeo hadi amalize haja yake kwani wakati mwingine huchelewa, ni bora kwa mwanamme ajipambe na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :

لا يؤمن أحدكم حتى يحبّ لأخيه ما يحبّ لنفسه

“Hatoamini mmoja wenu hadi ampendelee nduguye lile analolipendelea katika nafsi yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

na ukweli ni kwamba hakuna aliyekuwa karibu kufanyiwa hayo isipokuwa ni mke.

Tukiulizana ni vipi mwanamme anafika kilele cha ladha ya jimai? Utaona kwamba ufumbuzi unapatikana katika hali zifuatazo. Kuamini kuwa tendo la Ndoa ni Ibada:
                                                                                                                                                         

1. Tendo la Ndoa ni Ibada - النّكاح عبادة

Uislamu umenyanyua hadhi ya suala la tendo la ndoa na kulifanya kuwa ni ibada, ibada ambayo wana ndoa wakiifanya hulipwa. Kwani kwa ndoa yao hii ya halali wamejiepusha na maasi na uchafu na wakaishi katika sakafu moja katika mazingira ya kufahamiana, kupendana, kushibana na mahusiano mazuri ya kubadilishana mapenzi yenye kulandana.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  juu yake amani na salamu anasema:

في بضع أحدكم صدقة

“…na katika kumuingilia mkeo ni sadaka.”(Muslim)

Tendo la ndoa ni sadaka anayotoa mume kwa mkewe, na katika ukamilifu wa neema ni mtu kuhisi kuwa haja zake zinashibishwa na ndipo hapo nafsi inapopata utulivu na malipo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).

Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah)  anasema: kila ladha husaidia ladha ya siku ya mwisho, ladha hiyo hupendwa na Inaridhiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na mtendaji hupata ladha katika sura mbili:

Upande wa mwanzo ni kule kustarehe na kujifurahisha na kupata utulivu wa macho.

Upande wa pili ni kule kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  na huko ni  kuifikisha nafsi katika daraja la ladha iliyo bora zaidi.

                                                                                                                                                                 

2. Kubusu kabla ya Kuingiliana - القبلة قبل الجماع

'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  amesema:
“Hakika Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alikuwa akiwabusu wake zake kisha akitoka kuelekea kuswali na hakuwa akitawadha.”
(Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ahmad)

Tendo la kubusu lina athari muhimu sana katika mapenzi na hukurubisha zile hisia za mapenzi na mwisho hupelekea kugandana kwa kiwiliwili, na jinsi lilivyo muhimu ni kuwa mwenyewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikuwa haliachi hata kama amefunga saumu, kwani alikuwa akibusu na akiwakumbatia wake zake hali ya kuwa amefunga.” (Al-Bukhaariy na Muslim) Ummu Salama (Radhiya Allaahu 'anha)  amesema: Hakika Mtume wa Allah alikuwa akiwabusu wake zake hali ya kuwa amefunga.

Busu linakuwa katika hali nzuri na yenye kufidisha na kusisimua likiwa ni ndefu na haswa linapokuwa ni mdomo kwa mdomo hali ya kuwa wamefunga macho mawili na kufungua kidogo kidogo mara kwa mara. Wakati huo inapokuwa miili imegandana na pumzi kubadilishana hali zikiwa moto moto, ukianzia kuvuta kwa ndani kabisa na macho yenu yakiwa yanaangaliana kwa huruma. Yote haya huzipa raha nafsi za wanandoa na ni vitangulizi vizuri kwa kutayarisha mazingira mazuri ya kuanza kwa Jimai.

Kubusiana hakuishii katika midomo miwili tu, lakini huweza kuendelezwa katika maeneo mengine ya kiwiliwili ambayo yanaweza kusisimshwa na na hivyo  matamaniwa yakasimama.
                                                                                                                                  

3. Kuchezea Chezea Kinembe - دغدغة البظر

Kinembe ni moja katika maeneo muhimu sana ambayo yanaamsha hisia za jimai kwa mwanamke. Kukichezea kwa mwanamme ni muhimu sana ili kusisimsha hisia za kutamani kuingiliwa kwa mwanamke. Jinsi ya kukichezea inatakiwa iwe kwa upole na uangalifu mkubwa. Kinaweza kuchezewa kwa njia ya mkono au kwa njia ya kichwa cha dhakari ya mwanamme, na baada ya hapo ndipo anapoweza mwanamme kumuingilia mkewe na kukamilisha haja na matamanio yao.





Hali kadhalika inapendeza zaidi kwa mwanamke kuendelea kuchezewa kinembe hata baada ya kuingiliwa au Jimai kumalizika ili kumsisimsha zaidi na hivyo kufikia kileleni kama bado hajafikia alipokuwa akiingiliwa na mumewe.

                                                                                                                                                                                                               

4. Kutafuta Raha bila ya Jimai - الاستمتاع دون جماع

Je mwanamke akiwa katia udhuru, kwa kuwa ni mwenye hedhi, mwanamme huruhusiwa kumchezea mkewe? Au amtelekeze na kumtenga kabisa kwa sababu hiyo?

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  ana msemo maarufu kuhusu wanawake wenye hedhi, anasema:

اصنعوا كلّ شيئ إلاّ النّكاح

“Fanya kila kitu isipokuwa kumuingilia.”
(Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)

Na imepokewa kwa wake za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kuwa Mtume “Anapotaka kustarehe na mke wake mwenye hedhi basi hufunika tupu ya mwanamke.” (Abu Daawuwd). Na kutoka kwa Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  amesema: Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akimuamuru mmoja wetu akiwa na hedhi ajifunge shuka kwenye tupu yake kisha humchezea.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Mahusiano ya mke na mume hayaishii katika Jimai peke yake bali yanakusanya kuona raha katika uke wa mke na hisia nyingine za kibinaadamu kama vile kunusa, kukumbatia, na kuchezeana, michezo mingine ya kuchekesha na kushikana shikana kwa aina zote mbali na tendo lenyewe la Jimai. Na hii hufanikisha hamu na matamanio ya kubadilishana baina ya wanandoa wawili. Kwa mwanamke mwenye hedhi huku kutomaswatomaswa humsaidia kumpunguzia ule usumbufu aupatao katika hedhi yake na lingine muhimu zaidi ni kufahamu vile vile kuwa yeye si chombo tu cha kushibisha matamanio ya kingono ya mumewe peke yake bali kuna mambo mengine amabayo ni muhimu vile vile mbali na kule kushuka na kumwaga.


                                                                                                                                                          

5. Uhuru wa Kuangalia Uchi - حريّة النّظر إلى العورات

Baadhi ya Majahili hudhani kuwa kuanglia tupu ni haramu au makruhu, na kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  amekataza hilo na kulitahadharisha nalo watu, na wanapokea kwa Aisha kuwa amesema: sikupata kuona uchi wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  hata siku moja. Hadithi hii imebatilishwa na Haafidhw Ibn Hajar, kuwa ni uongo mtupu na imezushwa.

Na ndivyo hivyo imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kuwa amesema: “Atakapomuingilia mmoja wenu mke wake basi asimuangalie kwenye tupu yake kwani hiyo hupelekea mtu kuwa kipofu.” Na hadithi hii ni Mawdhuw' (imezushwa) kama alivyosema Ibn al-Jawziy na Abu Haatim alrRaaziy.

Na sisi hapa tunasema kuwa amepokea At-Tirmidhiy na Abu Daawuwd na wengineo kutoka kwa Mu'aawiyah bin Hayda amesema: nilisema: Ee, Mtume wa Allaah, uchi wetu, tunaingilia na kuangalia? Akasema:

احفظ عورتك إلاّ من زوجتك أو ما ملك يمينك

“Hifadhi uchi wako ila kwa mke wako au kwa wale unaowamiliki mkono wako wa kuume.”
 (Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ahmad)

Na hii ni dalili tosha ya kuruhusu kuangaliana uchi baina ya mke na mume.
                                                                                                                                                     

6. Kuondosha Nguo Zote - التجرّد من الملاب

Ukweli ni kuwa nguo zina nafasi yake katika kuonyesha uzuri na kusisimsha, na kuonesha mandhari nzuri kwa wanandoa wawili. Vile vile kama zilivyo nguo nzuri na zaidi, uchi huonyesha uzuri, husisimsha na huvutia katika kufanya kazi ya kuamsha hisia na matamanio.

Kama ilivyokuwa maarufu kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alivua nguo zake alipokuwa akioga sehemu moja na Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) . Tunachoweza kutolea dalili hapa ni neno lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Surat al-Baqarah Aliposema:

هن لباس لكم وأنتم لباس لهن

“…Wao ni (kama) nguo kwenu (zilizokugandeni mwilini), na ninyi ni (kama) nguo kwao…” (Al-Baqarah: 187)

Nako huku kuwa uchi kabisa kunapendezesha na kuwezesha kufikia kilele za raha za kimwili azipatazo mtu, hivyo basi hufanikisha kufikia lengo lililokusudiwa la kila mmoja wa wanandoa kuwa ni nguo kwa mwenzake!
                                                                                                                                  

7. Kuchezeana kwa Kuangaliana! - المداعبة عن طريق النّظر

Katika kuangalia kunaleta mvuto mkubwa katika moyo wa mwanaadamu na kunaamsha hisia kali za kimapenzi. Baadhi ya washairi wanaona kuwa kuangalia ni mshale unaoteka na kusibu lengo na kuua. Anasema mmoja wao:





Nami ninaona lau kama muangaliaji atawindwa


kwa kuangalia kwake mwanamke atakuwa ameniwinda


na kulisemwa zamani: muonaji ni bora ya muhadithiwa.





Kule kuona kunahadithia hisia za moyo wa mtu, na huelezea undani wa nafsi na kile ambacho nafsi imekibeba katika hisia za mapenzi ambazo zinapelekea kumsisimsha mtu na kudumisha ndoa.





Na ilikuwa ikisemwa hapo nyuma mambo manne hayashibishwi ila na mambo manne: Macho kwa kuona, mwanamke kwa mwanamme, Ardhi kwa kupata mvua na masikio kwa kupata habari.





Kuangaliana kwa wanandoa kunapelekea kukubaliana, kuvuta hisia, ambayo inapelekea katika mahaba na kuhurumiana. Hivyo tunaweza kuema Macho ni chanzo cha mvuto na kilele cha ladha ya mapenzi.





Na inatakiwa muono huu wa kuangalia uwe sio wa kukazia bali wa kuibia na kusinzia ili anaeonwa aingie haswa katika moyo. Antar kwa ushujaa wake na ugumu wa moyo wake katika kuua maadui zake anaelezea muono wa macho na athari yake kwa kusema:





Ee, wewe yule uliyetupa moyo wangu katika kupata


na kuufunika kwa mishale yenye sumu na kuuona kwake ugumu.
                                                                                                                      

8. Athari za Sauti na Harakati katika Kuchezeana - الحركة والصّوت أثناء المداعبة

Harakati zina athari kubwa sana katika kuonyesha uzuri wa mwanamke na haswa zaidi ule wa kiroho, kwani harakati za mwanamke zinachanganya akili ya mwanamme, na mshairi Umru al-Qais anayo haya ya kusema:





Ikiwa kelele imeondoshwa katika nguo yake


inapelekea katika ulaini kusikokuwa na ukali


kama mchanga uliojikusanya wanatembea wazazi wawili juu yake


kwa jinsi walivyojifikiria kwa ulaini wa mshiko na wepesi wake.





Sauti ni chemchem ya mvuto wa hisia kali za ladha na kimapenzi, vile vile ni chanzo cha kuzungumza maneno laini ya kimapenzi, na ndani yake ni dekezo na sisimko, na sauti ya mwanamke katika kilele cha ladha ya jimai inapendeza zaidi ikiwa ni laini yenye Naghma.





Mwanamke kwa uzuri wa harakati zake na uchangamfu wake na uzuri wa sauti yake na utamu wake humvutia mwanamme na huteka moyo wake. Hivyo basi kuchezeana kunawafikisha katika kilele cha ladha ya tendo la Jimai.





Katika wanawake kuna ambao wanatoa sauti zao wakati wa Jimai na hilo halina tatizo. Asyuuti ametaja katika kitabu chake (ad-Durrul al-Manthuur) kuwa Muawiya bin Abi Sufyaan alimuita siku moja mke wake (Fakhita), akaitikia mwitiko wa kusemea puani wenye matamanio ndani yake, akaona haya na kuhisi vibaya. Muawiya akamwambia: usijali, Wallahi wabora wenu ni huu mfano wako wenye kupiga ukelele kwenye mapenzi, kunguruma na kuzungumzia puani!


Na katika yote haya ni msisimsho na furaha ndani yake.



Share

9. Kulidekeza Jina la Mke - ترخيم اسم الزّوجة

Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alimuita 'Aaishah jina lake kwa kulidekeza na kumuita 'Aaishu. Na lengo la mwito huu ni kuonesha mapenzi kwa mke na kujikurubisha nae.

Hivyo basi ni juu ya waume kujifunza kutoka kwa kiongozi wetu pindi wanapocheza na wake zao, kwani katika haya ni raha tupu kwa yule atakaemudu kuifanya vizuri fani hii aliyotufundisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Na katika dekezo la namna hii ni kuonesha mapenzi ya kweli na inapelekea katika ladha na kusisimsha shauku na kuwafurahisha wote pamoja.
Share

ADABU ZA MAISHA YA NDOA - آداب الحياة الزّوجية

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema katika Surat Ruum Aayah ya 21:

ومن آياته أن خلق لكم من أنفسكم أزواجا لتسكنوا إليها وجعل بينكم مودة ورحمة إن في ذلك لآيات لقوم يتفكرون

“Na katika ishara Zake (za Kuonyesha ihsan juu yenu) ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofikiri.” (Ar-Ruwm: 21)

Katika Aayah hii kuna ishara katika misingi inayosimamisha maisha mazima ya mke na mume ambayo itapelekea katika furaha. Furaha ambayo itakuwa na misingi madhubuti ya mapenzi na huruma, mawaddatan warahmah.

Ni juu ya wanandoa wawili kuujenga vizuri uhusiano wao hadi ufikie katika sifa hii ya mapenzi (mawadda) wanapokuwa ni vijana, na kuhurumiana (rahma) wanapokuwa ni watu wazima.

Na katika jumla za adabu ya maisha ya ndoa ni:

                                                                                                               

1. Tabia Njema - حسن الخلق

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

وعاشروهن بالمعروف

“ … na kaeni nao kwa wema…” (An-Nisaa: 19)
katika Aayah nyingine ya sura hiyo hiyo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anaendelea kututanabaisha

وأخذن منكم ميثاقا غليظا

“…Nao wanawake wamepokea kwenu ahadi thabiti (kuwa mtakaa nao kwa uzuri).” (An-Nisaa: 21)
Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akielezea fadhila za tabia njema anasema:

أكمل المؤمنين إيمانا أحسنهم خلقا, وخياركم خياركم لنسائهم خلقا

“Muumini aliyekamilika kwa imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zake kwa tabia.”
(Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  amesema tena:

خيركم خيركم لأهله , وأنا خيركم لأهلي

“Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani (ahli).”
(Ibn Maajah na Ad-Daarimy)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

إنّ المرأة خلقت من ضلع وإنّ أعوج شيئ في الضّلع أعلاه , فإن ذهبت تقيمه كسرته , وإن تركته لم يزل أعوج , فاستوصوا بالنساء

Mwanamke Ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni (kuwafanyia wema) wake zenu.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Si hayo tu aliyohimiza Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kuhusu wanawake. Bali kwa umuhimu na unyeti wa suala hili tunaona kuwa katika usia wake wa mwisho anatuuusia:

الله الله في النساء فإنّهن عوان في أيديكم , أخذتموهنّ بأمانة الله , واستحللتم فروجهنّ بكلمة الله

“Allaah, Allaah, kwa wanawake, hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) (Iijaab na Qubuwl).” (Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad)

Na katika jumla ya tabia nzuri katika maisha ya ndoa ni kuacha kumfanyia mke maudhi ya aina yoyote ile. Vile vile kumfanyia na kumtendea mazuri, na kucheza nae na kuongea nae kwa upole. Hali kadhalika kujali zaidi uadilifu katika mambo yake na kufuata siasa za kati kwa kati katika muamala wako nae na haswa katika yale yenye maslahi kwake na yale yenye kuhifadhi akhlaq zake kulingana na haja, sehemu au tukio.
                                                                                                                                                                   

2. Kuishi nae kwa Wema hata Ikiwa Unamchukia - المعاشرة بالمعروف حتّى في حال الكراهية

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
وعاشروهن بالمعروف فإن كرهتموهن فعسى أن تكرهوا شيئا ويجعل الله فيه خيرا كثيرا
“ …na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu Ametia kheri nyingi kwake.” (An-Nisaa: 19)

Katika hilo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

لا يفرك مؤمن مؤمنة إن كره منها خلقا رضي منها آخر
“Habughudhiki muumini mwanamme kwa tabia ya mke wake akichukizwa na moja ( ya tabia) atapenda nyingine.” (Muslim na Ahmad)

Hata hivyo hakuna binaadamu aliyekamilika, anayeweza kusifika kwa ukamilifu wa tabia zote za kuigwa, na vile vile hakuna maisha yenye furaha yaliyokamilika. Hivyo basi ni lazima yawepo mapungufu na matatizo, ambayo yanahitajia suluhisho litakalofikiwa kwa ushirikiano wa pande zote mbili (mume na mke) ili kutatua na kuyashinda.

Katika kuamiliana na matatizo yanayojitokeza kunahitaji subira, uvumilivu na utulivu ili maisha yaweze kuendelea na mambo kuweza kurejea kama yalivyokuwa kabla.

Na katika matengamano ya maisha haya ya ndoa ni kuishi na mke kwa wema hata katika hali ya kuwa hata kama unamchukia. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  anatufundisha:

أن تطعمها إذا طعمت , وتكسوها إذا اكتسيت , ولا تضرب الوجه ولا تقبّح , ولا تهجر إلاّ في البيت
“Kumlisha unapokula, na kumvisha unapovaa, wala usimpige usoni na kumharibu na usimtusi (kwa matendo yake na maneno yake) wala usimhame kwenda nyumba nyingine (umhame kitanda tu).”
(Abu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad)

Na ni juu ya mwanamme yeyote kumtizama na kumuangalia mwanamke kulingana na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :

ارفق بالقوارير
“Wafanyieni wema vyombo vyenu (qawariira).” (Al-Bukhaariy)

Na usia huu unaohusu wema unakusudia upole na mazungumzo mazuri na kuvumilia maudhi. Hali kadhalika kumfanyia uadilifu katika hali zote.

                                                                                                                                                                   

3. Uwastani katika Wivu - الاعتدال في الغير

Huu uwastani unaokusudiwa hapa ni kutoghafilika na mambo ambayo matokeo yake huogopwa siku zote, na kutozidisha dhana na dhulma katika kuhesabu mambo.

Amesema mbora wa viumbe juu yake Swalah na amani:

إنّ من الغيرة غيرة يبغضها الله عزّ وجلّ وهي من غيرة الرّجل على أهله من غير ريبة

“Hakika katika wivu ni wivu unaombughudhi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  nao ni wivu wa mwanamme kwa mkewe katika kisichokuwa na shaka.” (An-Nasaa, Ibn Maajah na Ad-Daarimy)

Swahaba 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya AAllaahu 'anhu) anasema:

لا تكثر الغيرة على أهلك فترمى بالسوء من أجلك
                                                                                                                                                                                      
Msizidishe wivu kwa wake zenu ukaangukia  uovu kwako.”

Wivu unatakiwa na ni muhimu ili kulinda hadhi ya mtu na ikithibiti sehemu yake basi inapendeza na kupongezwa na shsri'ah, katika hili Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ana haya ya kusema:

 إنّ الله يغار , والمؤمن يغار, وغيرة الله تعالى أن يأتي الرّجل ما حرّم عليه
“Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Huona wivu na muumini huona wivu na Wivu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Unakuwa pindi mtu anapofanya alichoharamishiwa.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Leo hii watu ambao hudhani kuwa wamestaarabika huchukuwa wake zao wakiwa wamekamilika kwa mapambo yao huenda na kukesha na marafiki zake katika sehemu za starehe na wakati mwingine humtoa kwa aliyemuomba acheze na mke wake na hana wasiwasi kabisa, Je, huku si kufa kwa nafsi za wivu kwa watu hawa?!

Suluhisho la amani la tatizo hili ni kutochanganyika wanaume na wanawake. 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhu)  alikuwa siku moja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema: Ni kitu gani bora kwa mwanamke? Hawakujibu kitu na niliporejea nilimwambia Fatima: Je, ni kitu gani bora kwa mwanamke? Akasema: “Asifanyiwe rehani mumewe. Nikalitaja hilo kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) .”Akasema: “Huyo (aliyekuambia) ni fatima nae ni sehemu yangu (damu yangu).” (Al-Bazaar)

Ibn al-Qayyim amesema: Asili ya Dini ni wivu, na asiyekuwa na wivu hana dini, na wivu unalinda moyo na huo moyo unalinda kiwiliwili, hivyo basi huuzuia moyo kufanya uovu na uchafu. Na kukosekana kwa wivu hufisha moyo hivyo basi na kiwiliwili kizima hufa, hivyo anakosa kinga ya kujizuia na maovu na machafu.

Mfano wa wivu ni kama ile nguvu inayozuia maradhi na kuukinga mwili, hivyo kinga hiyo ikiondoka ugonjwa huingia sehemu ile ya mwili na hukosa cha kuizuia na kuilinda, hivyo ugonjwa hukaa, na hapo ndipo penye maangamizi yenyewe.


                                                                                                                                                              

4. Uwastani wa Kutoa katika Matumizi - الاعتدال في النفق

Ni kutofanya Israafu na kutokuwa bakhili, bali kinachohitajika hapa ni suluhisho la kati kwa kati nalo ni lile Analolisema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :

وكلوا واشربوا ولا تسرفوا إنه لا يحب المسرفين 

“ … na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri). Lakini msipite kiasi tu…” (Al-A'raaf: 31)

Na Maneno Yake Mengine Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

ولا تجعل يدك مغلولة إلى عنقك ولا تبسطها كل البسط

“Wala usiufanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo ovyo (utakuwa ni mwenye kulaumiwa ukifanya hivyo)…” (Al-Israa: 29)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema:

دينار أنفقته في سبيل الله , ودينار أنفقته في رقبة ,  ودينار تصدّقت به على مسكين , ودينار أنفقته على أهلك , أعظمها أجرا الذي أنفقته على أهلك

“Dinari utakayoitoa katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na dinari utakayoitoa katika kumkomboa mtumwa, na dinari utakayompa sadaka masikini, na dinari utakayoitoa kwa mke wako, bora ya dinari yenye malipo makubwa (katika hayo) ni ile utakayotoa kwa ajili ya mke wako.” (Muslim)

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema: “Atakapotoa mtu matumizi kwa mkewe, matumizi yaliyo katika hesabu itakuwa ni sadaka yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

Kitu muhimu kinachoangaliwa na Uislamu katika kutafuta riziki ni kuwa riziki yako ni halali na chanzo chake  ni halali ambayo haina uovu, shaka wala shubha ndani yake. Hili ni kwa hali yoyote ilivyo ya kimaisha na ugumu wake utakavyokuwa kwa kuingiliwa na mipenyo ya sheitani.

Hapa hatuna budi kumnong’oneza mke mnong’onezo ambao tunaufupisha katika haya: mume anaweza kupatwa na ufakiri hivyo ni juu yake awe na subira, kwani wewe ndie uliyemchagua kwa uhuru wako mwenyewe. Kisha elewa kuwa maisha ya kiuchumi ni yenye kubadilika, siku moja ipo pamoja nawe yaani maisha ya kiuchumi ni mazuri, lakini kumbuka vile vile kuwa siku nyingine maisha ya kiuchumi yanaweza kuwa magumu.

Ni uzuri ulioje mtu kutokufanya maisha yake kuwa makuu. Ajitahidi ayafanye mepesi yanayowezekana kuendeshwa bila matatizo yoyote na hivyi kumwezesha kuhifadhi kinachobakia. Ubadhirifu ni utazaa majuto, taabu na ubakhili. Bora ya mambo ni yale ya kati kwa kati. Tumuombe Allaah Atuondoshee kujiona, kujifakharisha na israafu. Aamiyn

5. Kujipamba kwa Ajili ya Mkeo - التزّيّن للمرأة

Hapana budi kwa wanandoa kujipamba na kuwa safi daima  kila mmoja kwa ajili ya mwenzake. Kujipamba huku ni kwa kuvaa vizuri na kujitia manukato.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

حبّب إليّ من دنياكم النّساء والطّيب
“Nimependezeshewa mimi katika dunia yenu wanawake na vitu vizuri vilivyosalimika na uchafu.” (An-Nasaaiy)

Kujipamba kunarithisha mapenzi na hujenga na kukuza sababu zote zinazopelekea katika kuzoeana. Kisha kumbuka, Allaah Hupenda yaliyo mazuri.” (Muslim na At-Tirmidhiy)

Ibn 'Abbaas (Radhi ya Allaah iwe kwake na baba yake) anasema: Mimi napenda kujipamba kwa ajili ya mke wangu kama nilivyokuwa napenda yeye ajipambe kwa ajili yangu.

Kujipamba ni haki ya wanandoa wote wawili mwanamme na mwanamke. Ni vizuri sana tusilidharau jambo hili la kujipamba na kuona si la muhimu kwani mwenye kuhitajia maisha ya furaha ya ndoa na yenye matokeo mazuri hana budi kujishughulisha na kijipamba.

6. Kumsaidia Mke katika Kazi za Nyumbani - مساعدة الزّوجة في الأعمال المنزلي

Amesema bibi 'Aaishah (Radhiya AAllaahu 'anha) :

قالت عائشة رضي الله عنها : كان صلى الله عليه وسلم يكون في مهنة أهله فإذا حضرت الصّلاة خرج إلى الصّلاة.
“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akiwasaidia katika kazi za nyumbani na inapowadia muda wa Swalah alikuwa akitoka kwenda kuswali.”
 (Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na Ahmad)

Na alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), “Akitoa uchafu katika nguo zake, na akikama mbuzi maziwa na akijuhudumia mwenyewe.” (Ahmad)
“Na alikuwa yeye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akishona nguo zake na kusafisha ndala zake.” (Ahmad)

Katika haya yote tunajifunza kutojikweza na tunahamasishwa kuwa na tabia nzuri za kusaidia katika kutunza nyumba na familia.
                                                                                                                              

7. Kukubali Kukosolewa na Mke kwa Moyo Mkunjufu - الاستماع إلى نقد المرأة بصدر رح

Walikuwa wake wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  wakijibizana wakati mwingine, na alikuwa akiwahama mmoja wao hadi usiku.

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  anasema kuwa kulikuwa na maneno baina yake na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) , akaambiwa 'Aaishah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : “Ni nani utakaemridhia baina yangu na yako?” (kusuluhisha) Je, utamridhia 'Umar? akasema 'Aaishah: Simridhii 'Umar kabisa, 'Umar ni mkali. Akasema tena Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : “Je, utamridhia baba yako baina yetu?” akasema 'Aaishah: ndio. Kisha akasema:” Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akatuma mtu aitwe Abu Bakr”, kisha akasema: “Huyu ana jambo na jambo  lake ni kadhaa.’ Akasema 'Aaishah: kisha akasema tena: muogope Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) , na useme haki tupu, akasema: akanyanyua Abu Bakr mkono wake, akampiga pua yake hata damu ikatoka- kisha akasema: huna mama Ee mtoto wa Ummu Ruumaan, unasema haki na baba yako na haki hiyo asiiseme Mtume wa Allaah. Anasema 'Aaishah: pua yake ikasimama utafikiri Swalah wawili hali yakimwagiwa maji kutoka katika kifuko cha maji na mfano wake. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kumwambia Abu Bakr: “Mimi sikukuitia hili.” Akasema 'Aaishah: kisha akasimama na kuchukua jarida lililokuwa nyumbani, kisha akaanza kumpiga nalo akageuka akamkimbia baba yake, akajificha nyuma ya mgongo wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) . Akaendelea kusema 'Aaishah: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akamwambia: “Nimekuapia ulipotoka, sisi hatukukuita kwa hilo (unalolifanya).” (Imefanyiwa takhrijy na Al-Haafidhw Ad-Dimashqiy)

'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) anahadithia kuwa kuna siku moja alikuwa ameghadhibika akamwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : “Wewe si unadai kuwa ni Mtume wa Allah! Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akatabasamu, na akalivumilia hilo kwa huruma na ukarimu.” (Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ahmad)

Mwanamke anaweza kumshupalia mumewe na akateleza katika haki ya mumewe nasi tuna mfano mwema wa kuigwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kwani yeye kwetu ni ruwaza njema na hakika ametufundisha jinsi gani ya kuamiliana. Katika misimamo na matukio kama haya, mwanamke ni sawa na mwanamme kwa kauli yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : Hakika wanawake ni ndugu wa wanaume.” (Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ahmad)

Ni bora zaidi kwa mwanamme awe ni mwenye kutumia akili zake vizuri kwa hekima na busara na haswa zaidi katika maeneo na matukio ambayo mwanamke atakuwa ameteleza na kupotea, ama akiyakabili makosa kwa makosa basi matokeo yake ni kuzidi na kupanuka tofauti hizi, na hili ni jambo lisilopendeza kabisa, na sio kwa maslahi ya wanandoa wawili.

                                                                                                                                                                   

8. Kujua Fiqhi ya Wanawake - الإلمام بفقه النسا

 Ni kitu kinachopendeza kwa mume kujua na kufahamu au hata kujifunza hukumu za ki-Fiqh zinazohusiana na wanawake, kwa khofu ya kutoangukia katika haramu, na amfundishe mkewe kama hafahamu hukumu za twahara na Swalah na hedhi…
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

يا أيها الذين آمنوا قوا أنفسكم وأهليكم نارا وقودها الناس والحجارة

“ Enyi mlioamini! Jiokoeni Nafsi zenu na watu wenu, na moto ambao kuni zake ni watu na mawe…” (At-Tahrym: 6)


Na ikitokea mwanamke hafahamu hukumu hizi za ki-Fiqh, au mumewe hakuweza kumfundisha ni juu yake kuwauliza Ahlu-Dhikri (wenye ujuzi) katika mabaraza ya ki-elimu yanayo jihusisha na wanawake.


Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

نعم  نساء الأنصار لم يمنعهنّ الحياء أن يتفقّهن في الدّين

“Wabora wa wanawake ni wanawake wa ki-Answaar ambao haikuwazuia haya katika kujifunza mambo ya Dini.” (Al-Bukhaariy na Muslim)
                                                                                                                                                                   

9. Asimgongee Mwanamme Kumgongea Mke wake Usiku: - ألاّ يطرق الرجل أهله لي

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik:

 أنّ النبي صلى الله عليه وسلم كان لا يطرق أهله ليلا كان يدخل غدوة أو عشاء
Kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alikuwa hagongi kwa mkewe usiku, alikuwa akiingia asubuhi sana au ishaa.” (Al-Bukhaariy na Ahmad)

Kutoka kwa ibn Umar (Radhiya Allahu 'anhuma) anasema kuwa:
وعن ابن عمر أنّ رسول الله صلى الله عليه وسلم نزل العقيق فنهى عن طروق النساء , فعصاه رجلان , فكلاهما رأى ما يكره.
“Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alishukia alghaqiiq akakataza kugongewa wanawake, watu wawili wakamuasi (wakenda kugonga kwao) na wote wawili waliona mambo yaliyowachukiza.” (Ahmad)

Hali kadhalika kutoka kwa 'Abdullaah bin Rawaaha kwamba siku moja alikuwa amerudi kutoka safari akachelewa, na akaona nyumbani kwake pana waka taa, na mke wake anacho kitu pamoja nae, akaamua kuchukua upanga, akasema mkewe: koma usinisogelee, ni mwanamke Fulani ananisuka, akajiwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  katika hilo na akakataza wanaume kuwagongea milango wake zao usiku. (Ahmad)
Share

10. Baina ya Wakwe na Mke wa Mtoto Wao - بين الحماة والكنّة

Uislamu umefaradhisha kuwepo kwa maisha mema na kutendeana vizuri katika muamala familia, na akajaalia misingi ndoa ni mapenzi na kuhurumiana. Hivyo basi hapana budi kuwasiliana na kuoneana huruma pamoja na wengine ndani ya familia, na haswa zaidi jamaa zake mume na jamaa zake mke.
Na ajitahidi sana mke kutokuufanya moyo wa mume wake kuwa mgumu sana kwa ndugu za mume wake, na kufanya mambo mabaya ili mume awachukie ndugu zake ni kumuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) . Kuvunja udugu ni jambo lenye kuchukiza na huondosha mahusiano ya ki-dugu, na vile vile huufanya moyo wa mtu kuwa ni mgumu na huvunja kabisa sababu za kuwasiliana. Wake zetu ni taa za njiani na ni nuru ya maisha na wala sio moto uunguzao au mwiba unaochoma. Ni juu ya wanandoa kusoma Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) inayosema:
وقضى ربك ألا تعبدوا إلا إياه وبالوالدين إحسانا
“ …na Mola wako Amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (Ameagiza) kuwafanyia wema  (mkubwa) wazazi”. (Al-Israa: 23)
Furaha ya ndoa inapatikana na kukua na inaendeelea kukua kadri mke atakavyomsaidia mumewe juu ya wajibu wake na kudumisha mahusiano yake (mke) nae na ya wengineo.
Mwanamke ni msaidizi wa mwanamme katika kumsaidia kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  na kuwafanyia wema, upole, na kuwanyenyekea wazazi, ndugu, wake na waume wa watoto wao.
Uislamu unatahadharisha katika ufanyaji dhulma na udikteta  na huu ni mlinganio katika kusimamisha amani ya kudumu baina yake mzazi wa kike au wa kiume na mke wa mtoto wao wa kiume (ambae ni kama mtoto wake wa kuzaa) na inabidi kuamiliana nao kwa upole na kwa ukarimu na hapo ndipo yatakaposimama mahaba na kutengemaa kwa familia.

*********************************************************************************

No comments

Powered by Blogger.