tafsir surat nnas 114.
114. SURAT ANNAS
(TAFSIRI)
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu,
2. Mfalme wa wanaadamu,
3. Mungu wa wanaadamu,
4. Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas,
5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,
6. Kutokana na majini na wanaadamu.
MAELEZO.
Sura hii iliteremka Makka.
Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamuamrisha Nabii wake s.a.w. amwendee Yeye amwombe ulinzi kumkinga na shari kubwa zinazo washinda watu wengi kuzitambua kwa sababu zinatokana na matamanio yao, na pumbao lao, basi wakatumbukia katika yale yale wanayo katazwa.
Hiyo ndiyo shari ya wasiwasi wa Shetani, anaye jificha machoni, au hujidhihirisha kwa kificho;
wasiwasi wake ni kwa hila na khadaa.
UFAFANUZI KWA KILA AYA.
1. Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha mambo yao
2. Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote wafalme wao na raia.
3. Mungu wa wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa ukamilifu atakavyo.
4. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma ukiomba msaada kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake.
5. Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.
6. Kutokana na majini na wanaadamu.
No comments